Skip to main content
Habari na Matukio

Taasisi za Wizara ya Kilimo zatakiwa Kupunguza na Utegemezi

Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika zimetakiwa kuwa na mikakati ambayo itaziwezesha kujitegemea katika  shughuli zao  ili kupunguza utegemezi katika mfuko wa serikali.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wizara ya kilimo chakula na ushirika Bibi Sophia Kaduma katika Kikao  kilichojumuisha Wakuu wa taasisi hizo  kilichofanyika katika ukumbi wa Kilimo I hivi karibuni
Akiwasilisha taarifa yake Bibi Sophia amezitaka kila Taasisi kuainisha vyanzo vyake vya mapato nje ya ruzuku  ya serikali  ikiwemo michango ya wadau .

‘kila Taasisi kwa namna moja au nyingine inakusanya mapato yake, “nataka kila mkuu wa Taasisi aainishe  vyanzo vyake vya fedha anavyotegema kukusanya katika mwaka 2014/15” alisema Bibi Kaduma.

Aidha katika kikao hicho wakuu wa taasisi walipata fursa ya kubadilishana uzoefu wa namna bora ya kuendesha taasisi hizo pamoja na ubunifu wa kujipatia fedha kutokana na rasilimali zake.  
Pamoja na hayo Katibu Mkuu alisisitiza kuwa vikao vya namna hiyo vitakuwa vinafanyika angalau kila robo mwaka ili kuongeza ufanisi katika kusimamia taasisi hizo.