Skip to main content
Habari na Matukio

Tanzania Kuwa Kinara wa Pamba

Tanzania imejipanga kuwa kinara wa uzalishaji wa pamba Barani Afrika ifikapo mwaka 2021 kutokana na mikakati ya uzalishaji wa mbegu bora ya zao hilo ambazo zimekwisha fanyika.

Akionea katika Kongamano la  Wadau wa Pamba lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina uliopo Dodoma Waziri wa Kilimo Mhe. Mhandisi Dkt John Tzeba  amesema mikakati ya kuongeza tija katika zao la pamba imeshafanyika ili kuboresha zao la pamba na kupunguza kodi  zinaongeza gharama za uzalishaji.

Akijibu hoja ya baadhi ya wafanyabiashara wa zao hilo waliolalamikia kodi katika mafuta ya pamba Mhe. Waziri wa Kilimo amesema Serikali imeaanda Kikosi kazi kinachowahusisha Makatibu Wakuu ili kuangalia kodi ambazo hazina tija ziweze kuondolewa katika utaratibu uliopangwa.

“Kwa mwaka huu kutakuwa na kiasi kikubwa sana cha pamba  kutokana na hali ya  uzalishaji ilinavyooneka  na huu ni mwanzo mzuri mpaka kufikia mwaka 2021 tutakuwa tunaongoza kuwa wazilishaji wakubwa wa pamba” alisema Mhe. Tzeba

Aidha amesisitizia wakulima kuacha kuuza  pamba ghafi ili kuimarisha soko la ndani na kuingizia taifa kipato hivyo kuwataka wakulima kulima kibiashara ili kupata soko la uhakika.

Pamoja na hayo Dkt. Tzeba amesema zaidi ya asilimia 95% ya pamba inayozalishwa hapa nchini inauzwa nje ndio maana soko la zao hili haliaminiki kwa kiasi kikubwa.

Awali  wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mhe. Mwijage anasema Sekta hii inahusisha mnyororo mrefu wa uongezaji thamani kuanzia kuchambua pamba (ginneries); kusokota nyuzi (spinning); kuseketa vitambaa (weaving); kufuma vitambaa (knitting), kuchapa na kutia rangi (processing) na kushona mavazi (garments) hivyo ina weza kuongeza ajira kwa kiasi kikubwa sana.

 

“Sekta hii ni muhimu katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuanzisha viwanda vinavyoajiri watu wengi kwa wakati mmoja. Aidha, Sekta hii itawezesha kupunguza uingizaji wa nguo kutoka nje na kuongeza matumizi ya pamba inayolimwa nchini pamoja na malighafi nyingine kama vile magadi na gesi asilia zinazopatikana nchini”.Alisisitiza mhe. Mwijage

 

Hata hivyo ameongeza kwamba Tanzania ina jumla ya viwanda 11 vya nguo na mavazi vinavyofanya kazi kwa sasa kati ya viwanda 16. Viwanda hivi vinatumia wastani wa asilimia 50 ya uwezo wake wote.

 

 

kuongoza katika uzalishaji wa pamba namba moja baarani afrika ifikapo mwaka  2021  kuwa mzalishaji na muuzaji wa pamba  namba moja kwa kiasi kikubwa