Skip to main content
Habari na Matukio

Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi

Uzinduzi rasmi wa Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi ulifanyika tarehe 27 Mei, 2017 katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi uliopo mjini Dodoma. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Charles J.Tizeba (Mb).

Baada ya uzinduzi huo wadau wanaweza kupakua Mwongozo na Wasifu kupitia tovuti ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (www.kilimo.go.tz) na kuvitumia katika kuwekeza na kuendeleza kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi hapa nchini.

Mwongozo na Wasifu huo umepatikana kutokana na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Wabia wa Maendeleo ( (FAO, DFID, WB, CIAT, Sekta Binafsi na Asasi zisizo za Kiserikali za kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika kuongeza usalama wa chakula na lishe hapa nchini.

Pakua Faili: