Skip to main content
Habari na Matukio

Wabia wa Maendeleo watia sahini kuisaidia SAGCOT

Wabia wa Maendeleo wakiongozwa na Bwana Philippe Dongier, Mkurugenzi Mkazi wa Bank ya Dunia nchini, leo wametia sahini ya makubaliano ya kuisaidia SAGCOT, makubaliano hayo ni utekelezaji wa ahadi za wabia hao ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Mpango huo.

SAGCOT ni kifupi cha maneno, chenye maana ya Southern Agricultural Growth Corridor Growth of Tanzania tafsiri yake ni Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini ilianzishwa miaka mitatu iliyopita leo lake kubwa na kusaidi uwekezaji mkubwa na mdogo katika kilimo kwa kushirikiana na sekta binafsi.

Awali katika hotuba yake ya ufunguzi wa tukio hilo, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Bibi Sophia Kaduma alisema kutiliana sahini ni mwanzo mzuri, kwani Serikali kwa kushirikia na sekta binafsi, maendeleo katika sekta ya kilimo yatafikiwa kwa haraka.

Bibi Kaduma alisema, lengo la Serikali ni kupunguza umaskini, kuboresha maisha ya watu vijijini na mijini na kuongeza kuwa kiasi cha dola bilioni 2.1 za Marekani ambazo zitawekezwa kupitia Mpango huo zitachangia katika ukuaji wa uchumi kupitia kilimo.

Naye Bwana Vel Gnanendran, Mwakilishi wa Mkazi wa DFID alisema huu ni mwanzo mzuri na tukio la kutiliana sahini ni mwanzo mzuri na kwamba wabia wa maendeleo wapo mstali wa mbele kuhakikisha, malengo ya SAGCOT yanafikiwa ikiwa ni pamoja na kuboresha utendaji kazi wa Mpango huo.

Bwana Geoffrey Kirenga, ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa SAGCOT alisema, Mpango huo unatekelezwa kwa pamoja kati Serikali kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo na kuishukuru Serikali kwa kuja na mtazamo mpya wa kuishirikisha Sekta binafsi katika kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa.

Bwana Kirenga aliongeza kuwa, sasa ni wakati wa kila Mtanzania kubadili fikra kwa kuwa, maendeleo yanaletwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi, na kushauri Watanzania kuacha fikra za kusubiri kusaidiwa. Bwana Kirenga alisema mpaka sasa, wabia wa maendeleo wametoa ahadi ya kiasi cha Dola za Kimarekani, bilioni 1 ambazo zitatolewa punde ili kuanza utekelezaji katika eneo la usimamizi na uratibu wa shughuli za SAGCOT.