Skip to main content
Habari na Matukio

Wadau Waombwa Kufadhili Mradi wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi

 

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo ameomba wadau wa Kilimo   kufadhili mradi wa  kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiathiri kilimo hapa nchini.

Akiongea wakati wa kikao cha wadau kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Serena iliyoko mjini Dar es salaam amesema kwamba mradi huo ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho mvua hazitabiriki ambapo utasaidia kubadilisha hali ya kilimo kwa kuwajengea uwezo wakulima katika maeneo yaliothiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Aidha prof. Amesema kwamba mradi huo unagharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 60 ambapo dola milioni 30 zitatolewa na mfuko unaofadhili kilimo (GCF) na dola za kimarekani milioni 30 zinatakiwa kutolewa na serikali au wadau wengine.

“Tumewaita ili tuweze kujadili namna ambavyo tunaweza kushirikiana nanyi katika kuchangia kiasi hicho cha dola milioni 30 ili tuweze kuwasaidia watanzania kupitia mradi huu wa kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia ya nchi” ,alisema Prof Tumbo

Mkuatno huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo NEPAD, GCF, SUA FAO DFID ICRAF CARE na International na wawakilishi wa wizara mbalimbali  ambapo walionesha nia ya kuchangia kwa namna yeyote mradi huo.

Aidha Prof Tumbo alisistiza kwamba  kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Taifa limechukua tahadhari na hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa Programu ya  Kitaifa ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi

Michango ya Kitaifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Nationally Determined Contributions) ya mwaka 2016  iliyowasilishwa kwenye Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi alimalizia prof.Tumbo.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mazingira Wizara ya Kilimo  Bi Shekwanande Natai amesema mradi huo ukipata fedha utasaidia wakulima zaidi ya milioni 1.5 katika mikoa  saba (7) ya Tanzania bara na mine (4) ya Zanzibar

Mikoa itakayofaidika na mradi huu kwa tanznia bara ni Arusha, Dodoma,Kilimanjaro,Manyara,Singida, Shinyanga na Tabora na kwa Zanziba ni Unguja Kaskazini,Unguja Kusini Pemba Kaskazini na Pemba kusini alisistitiza mama Natai.

Awali mama Natai amesema kwamba  mradi utasaidia kujenga uwezo na  kuondoa udhaifu uliopo katika  utunzaji aridhi ya kilimo pamoja na uwezo mdogo wa kukabiliana na athari za tabianchi.

Amesema kwa kupitia mradi huo wakulima na wafugaji watapa elimu juu ya uapatikanaji wa mitaji na masoko ya bidhaa zao  na sekta biafsi itaweza kushiriki kikamilifu katika kupambapana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwongozo wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi umeandaliwa kutokana na nyaraka zinaoonyesha dhamira ya Serikali za kufanya sekta ya kilimo iweze kuhimili mabadiliko ya tabianchi hadi kufikia mwaka 2030 alimalizia mama Natai.

Elirehema Swali ni moja ya watafiti ambao wameshughulika na uaandaaji wa maradi wa mradi huo utashughulikia uongezaji wa thamani  katika mazao ya mafuta  kama alizeti na mazao ya nafaka kama mtama

Alienedelea kusema kwamba Mahitaji ya Utekelezaji na Uendelezaji wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi yanahusisha uboreshaji uzalishaji na kuongeza tija, kujenga ustahimilivu wa kukabiliana na  mabadiliko ya tabianchi

Bwana Elirehema Swali alibainisha kwamba katika wasilisho lake kwamba mradi utasaidia Kuunganisha mnyororo wa thamani Utafiti kwa ajili ya maendeleo ya kilimo na Kuimarisha na kuendeleza huduma za ushauri wa kilimo pamoja na Utabiri wa hali ya hewa.

Mwisho