WAHARIRI WASHUHUDIA UTEKELEZWAJI WA MIRADI YA KILIMO NCHINI
Ni mwaliko wa Waziri Bashe mkoani Dodoma.
Na Evance Ng’ingo
VYOMBO vya habari ni kati ya nyenzo sahihi na muhumu inayotumiwa katika kuifikia jamii kwa haraka huku ikiwasilisha taarifa lengwa kwaufanisi, iwe katika nyanja za afya, elimu, biashara, kilimo na nyinginezo.
Katika kutambua hilo Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe mnamo Januari 10, mwaka huu jijini Dodoma alizungumzana Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari na kuwaelezea mafaniko ya utekelezwaji wa vipaumbele vya sekta ya kilimo anayoiongoza.
Wahariri aliokutana nao ni kutoka katika Magazeti, Radio, Luninga na mitandao ya kijamii ambapo mbali na wahariri hao kuzungumza na Waziri Bashe siku hiyo, siku moja kabla ambayo ni Januari 9 walipatiwa elimu kuhusiana na Sumu Kuvu kutoka kwa wataalamu mbalimbali, semina iliyoandaliwa na mradi wa Tanipac. Na Janauri 11 wakatembelea kiwanda cha kuzalishia mbolea cha Itracom kilichopo Nala- Dodoma.
Hotuba ya Waziri Bashe Januari 10:
Wakiwa kwenye ukumbi wa Mabele- Dodoma walisikiliza hotuba ya utekelezwaji wa vipaumbele vya Wizara ambapo Waziri Bashe alitumia takribani saa moja na dakika 45 kufafanua namna ambayo wizara yake inatekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya kilimo.
Waziri Bashe kati ya masuala aliyogusia kwenye hotuba yake ni pamoja na Miradi ya Umwagiliaji, Mashamba Makubwa (Block Farming),
Uimarishwaji wa Huduma za Ugani, Utafiti, Uuzwaji wa Bidhaa za Mazao nje ya nchi.
Pia aligusia kuhusiana na uzalishwaji wa mbegu nchini, uboreshwaji wa mazao ya Pamba, Alizeti, Korosho,kahawa na mengineo mengi.
Pia aligusia masuala mengine mtambuka ambayo wizara imekuwa ikitekeleza yenye kulenga kuinua sekta ya kilimo kama vile kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye kilimo pamoja na kuwawezesha vijana kushiriki kwenye kilimo kupitia mradi wa Building Better Tomorrow.
Waziri Bashe pia amesema“Vyombo vya habari ni kati ya nyenzo muhimu katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini hasa kutokana na uwezo wake wa kuifikia jamii kubwa iwe ndani na nje ya nchi, ninawaagiza Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara kushirikiana kikamilifu na vyombo ya habari hasa kwa kuwapatia taarifa wanazotaka kwa wakati.”
Semina ya Sumu Kuvu,
Siku ya Januari 9, Wahariri walipatiwa mafunzo kuhusiana na Sumu Kuvuambapo wakufunzi mbalimbali walitoa mada kuhusiana na madhara ya Sumu Kuvu, namna ya kuidhibiti pamoja na njia za kujilinda isitokee.
Pia walielimishwa sababu za kutokea kwa Sumu Kuvu na mbinu za kuandikahabari za kuielimisha jamii kuhusiana na Sumu Kuvu bila ya kusababisha hofu au kupotosha.
Kutembelea kiwanda cha Itracom
Kiwanda hicho cha kuzalisha mbolea kilichopo eneo la Nala nje kidogo ya Jiji la Dodoma ni cha mwekezaji kutoka nchini Burundi aliyevutiwa na sera nzuri za uwekezaji za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kampuni.
Kwa sasa kimeshaanza uzalishaji ambapo wahariri walipata wasaha wa kujionea mashine za kisasa za kuzalishia mbolea, eneo la kuhifadhia malighafi ya mbolea na walizungumza na watendaji mbalimbali wa kiwanda hicho.