Skip to main content
Habari na Matukio

Wakulima waaswa juu ya Sensa ya maendeleo ya Kilimo

Wakulima na wadau wa Kilimo wameaswa kutopuuza zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 26 mwez huu. Wito huo ulitolewa na  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal katika kilele cha sherehe sikukuu ya wakulima Nane nane iliyofanyika katika viwanja vya Zuguni, mjini Dodoma.

Aidha Dkt Bilal aliwataka wakulima pamoja na wadau wote wa Kilimo kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa Sensa ili kufanikisha zoezi hilo muhimu.

“Sensa  ni muhimu katika maendeleo ya nchi na pamoja na watu wake kwani inawezesha Serikali na wadau wake kupanga mikakati sahihi ya maendeleo kwa manufaa ya wote”, Alifafanua Dkt Bilal.

Hata hivyo Dkt Bilal alifafanua kuwa  katika  Sekta ya Kilimo hutoa fursa ya kutambua idadi ya  wakulima na wadau wote wanaotoa huduma katika sekta ya Kilimo ili kupanga mipango katika kuboresha sekta hiyo.

Katika hotuba aliyoitoa Dokta Bilal katika maadhimisho hayo aliwataka wakulima na wadau wengine wa Kilimo kutumia nafasi hiyo muhimu  walionao hasa wakiwa ni sehemu kubwa ya Watanzania  kutoa maoni katika kufanikisha zoezi la ukusanyaji maoni kwa ajili ya Katiba mpya.