Skip to main content
Habari na Matukio

            Wakulima Wavutiwa na Mbegu Bora za Mpunga

Wakulima Mkoani Morogoro wamevutiwa na mbegu mpya za mpunga ambazo zinastawi nchi kavu,zinachukua muda mfupi kukomaa na zina mavuno mengi.

Ufanisi wa mbegu hizo ulionekana  katika mashamba darasa ya mpunga katika Vijiji vya Kisaki,Tawa,Msonge,Tawa,Kiloka,Dala na Mtamba katika Halimashauri ya Mororogoro vijijini ambapo wakulima wa maeneo hayo walifanya majaribio ya aina nne za mbegu za mpunga

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa Siku ya Mkulima iliyofanyika katika  kijiji cha Mtamba hivi karibuni na kuhudhuriwa na viongozi wa  ngazi ya Mkoa Wilaya pamoja na Vijiji  wakulima hao wamesema, mbegu aina ya Nerika 1,Nerika 2 Nerika 4 na Nerika 7 zinapendwa na wakulima kutokana na uwingi wake wa mazao kwa ekari pamoja na muda mfupi wa kukomaa

Hamisi Mfaume ni mkulima wa kiongozi wa kijiji cha Kisaki Morogoro Vijijini anasema majaribio ya mbegu walioyafanya katika mashamba manne tofauti ambapo imeonekana dhahiri kuwa mbegu hizo zina ufanisi mkubwa

‘ ulifanya majaribio katika mashamba  manne tulikopanda  aina nne za mbegu ambazo zilikuwa ni Nerika 1  inachukua kati ya siku 95-100,na hutoa kilo 1800 kwa heka moja.Nerika 2 huchukua siku 90-95 toka kupandwa hadi kuvunwa na hutoa kilo 1600 kwa ekari moja,wakati Nerika 7 inatoa kilo 2000 kwa ekari moja na huchukua siku kati ya 95 mpaka 100’. Alisema hamisi mfaume

Aidha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa uzalishaji wa mbegu za kilimo (ASA) Dr.Filimini Mizambwa amewataka wakulima  kuchagua aina moja au mbili ya mbegu hizo ambazo wanazipenda ili kuwa na aina moja  ya uzalishaji wa mpunga unaofanana katika eneo moja.

Aidha Dr. Mizambwa aliwataka wakulima hao viongozi kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wengine ili kuongeza uzalishaji na kuimarisha usalama wa chackula nchini.