Skip to main content
Habari na Matukio

WANANCHI WA SINGIDA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUANGAMIZA KWELEAKWELEA.

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Vijjiini wameipongeza Serikali kwa zoezi la kunyunyiza sumu ya kuua ndege waharibufu aina ya kweleakwelea.

Akizungumza kabla ya  kuanza kwa zoezi la kuangamiza kweleakwelea katika katika eneo la Barangida mpakani mwa miloa ya Singida na Manyara mkulima  Grabriel Said  wa kijiji cha Pohama kata ya Ngimu amesema hatua ilichukuliwa na Serikali imemfurahisha kwani imemrudishia matumaini ya kuvuna.

"Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwani serikali imesikia kilio chetu imeleta hii ndege ya kunyunyiza kiwatilifu  kuangamiza kweleakwelea". Amesema Bwana Said.

Kwa upande wake mkulima Hussein Juma  kutoka kijiji cha Mtambaa amesema  anamshukuru sana Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe kwa kuwapelekea huduma ya kuangamiza kweleakwelea kwani ameshaanza kuona matokeo mazuri baada ya  makundi ya kweleakwelea kuanza  katika maeneo anapofanyia shughuli za kilimo.

Akito tathimini ya zoezi la kungamiza kweleakwelea, Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya  Singida Natalia Mosha amesema zozi hilo lilianzia kijiji cha Merya kata ya Merya na litakua endelevu hadi kweleakwelea watapoangamizwa.

Amesema kata zilizoathiriwa zaidi ni Merya, Itaja, Ngimu na Mihunga.

Naye Afisa Kilimo  wa Kanda ya Kati kutoma Kitengo cha Afya na Mazao, Laurent Zumba amesema zoezi hilo  limefanyika kwa kutambua maeneo wanayolala na muda sahihi wa kunyunyizia ni  wakati wa jua kuzama.

Ameongeza kuwa kweleakwelea ni ndege wanaopenda kushambulia mazo ya nafaka zikiwemo mpunga,ngano, mtama na uwele.

Aidha ndege hao hulala maeneo tofauti na wanayotafutia chakula hivyo inahitaji uchunguzi ili kubaini maeneo wanayolala.

Kuhusu uwezo wa kusababisha hasara Bwana Zumba  mesema  kweleakwelea mmoja anauwezo wa kushambulia kati ya gramu tano hadi kumi za nafaka  kwa siku hivyo wanapoingia shambani kwa makundi humuweka mkulima kwenye hatari ya kupata hasara kwa asilimia mia moja.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inaendesha zozi la kuangamiza ndege aina ya kweleakwelea katika mikoa yote mbayo wananch wameripoti kuwepo kwa makundi ya ndege hao waharibufu.