Skip to main content
Habari na Matukio

Watumishi wampokea kwa furaha Naibu waziri Dkt Mary Mwanjelwa

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Eng. Methew Mtigumwe leo amewaongoza  Watumishi wa Wizara ya Kilimo kumpokea Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Mary Mwanjelwa ambaye ameteuliwa hivi karibuni kushika nafasi hiyo.

Katika uteuzi huo uliotokana na mabadiliko ya Baraza la Bawaziri la hivi karibuni ilitangazwa kuwa Waziri wa Kilimo ni Dkt. Charles Tizeba na Naibu wake Dkt. Mary Mwanjelwa.

Aidha Dkt Mary Mwanjelwa alipokelewa katika viwanja vya  Kilimo I kuanzia mida ya saa nne ambapo alikutana na viongozi waandamizi wa wizara  na watumishi wengine wote

Baada ya kutoka katika viwanja hivyo Naibu Waziri alipata nafasi ya kuongea na Wakuu wa Idara na Vitengo katika mkutano uliongozwa na Katibu Mkuu Eng. Methew Mtigumwe

Akiongea na wakuu wa Idara hao katika Ofisi ya Katibu Mkuu, Dkt Mwanjelwa ameomba ushirikiano kutoka kwa Wakurugenzi pamoja na Watumishi wengine ili kuweza kurahisha shughuli za wizara wanayoiongoza.
Dkt. Mary Mwanjelwa aliapishwa tarehe 9 Oktoba  kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo kutokana na  mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni, kabla ya uteuzi  huo  alikuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya