Skip to main content
Habari na Matukio

Waziri Afanya Ziara Mkoani Mbeya

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika amefanya ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya kukagua shughuli mbalimbali za kilimo mkoani humo, akiwa wilayani mbarali waziri aliwataka watendaji wa Halmashauri kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Vilevile ameagiza kuundwa kwa timu ya wataalamu kuchunguza sababu za kubomoka bwawa la lwanyo lilopo katika kata ya Igurusi wilayani mbalali.

Akiwa wilayaniMomba aliwataka wanakijiji wa kijiji cha Ukwile kata ya Isandula kutumia fulsa ya mipaka ya nchi za jirani kama Malawi na Zambia katika kupata masoko ya mazao yao pia Halmashauli na sekta binafsi kutatua changamoto za fedha zinazowakabili.

Waziri akiwa wilayani Mbozi alikagua maendeleo ya ununuzi wa mahindi unaofanywa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Wilayani humo.