Skip to main content
Habari na Matukio

WAZIRI BASHE AKUTANA NA DIAMOND OFISINI KWAKE

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na Msanii wa Muziki , Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz  ofisini kwake jijini Dodoma.

Mazungumzo ya Mhe. Bashe na Diamond yalihusu uwekezaji kwenye Sekta ya kilimo.

Katika mazungumzo hayo ambayo  yalihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Usimamizi wa Matumizi ya Ardhi ya Kilimo, Mhandisi Juma Mdeke na Mratibu wa Mradi wa Kilimo kwa Vijana wa Jenga Kesho yako(BBT) Vumilia Zenkankuba Diamond alimueleza Waziri Bashe nia yake ya kuwekeza kwenye kilimo.

Waziri Bashe amemwelezea Diamond utayari wa Wizara ya Kilimo katika kufanikisha uwekezaji wake kwa kumpatia ushauri  wa kilimo ikiwa pamoja na kumpatia wataalamu wa kilimo watakaompimia afya ya udongo ili kubainisha mazao sahihi ya kulima.

"Kilimo ni uwekezaji ambao una faida ya muda mrefu na nikuhakikishie Wizara itakusaidia vilivyo kukuwezesha kunufaika  uwekezaji wako kwa kukutanisha na wawekezaji wengine wakubwa ambao ni wanufaika kwenye mnyororo wathamani katika kilimo kama vile uzalishaji wa mbegu." amesema Waziri Bashe.

Wwa upande wake Diamond ambaye pia mmiliki wa kampuni ya Wasafi Media, Wasafi Betting na Kampuni ya kusimamia wasanii amemwelezea Waziri Bashe kuwa anatambua fursa nyingi zilizopo kwenye kilimo ambazo zimetokana na uwekezaji mkubwa wa Rais Samia Suluhu Hassan hivyo ameamua kujikita ili kutengeneza ajira zaidi kwa vijana na wananchi kwa ujumla.