Skip to main content
Habari na Matukio

Waziri Hasunga akabidhi taarifa ya ubadhilifu kwenye Vyama vya Ushirika kwa TAKUKURU

Waziri Hasunga akabidhi taarifa ya ubadhilifu kwenye Vyama vya Ushirika kwa TAKUKURU

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo amekabdihi ripoti ya ukaguzi wa Vyama vya Ushirika yam waka 2018/2019 kwa Kamishina Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o katika Ofisi za Wizara ya Kilimo, Mtumba Jijini Dodoma.

Mhe. Hasunga amesema ukaguzi uliofanya na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) umebaini ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Bilioni 124.5 ambapo umefanywa na Vyama Vikuu vya Ushirikia, Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS), Vyama vya Msingi vya Mazao (AMCOS) ambapo jumla ya vilivyokaguliwa ni hadi tarehe 30 Juni 2019 ni 11,410 kati ya Vyama hivyo, Vyama hai ni 6,463; Vyama Sinzia ni 2,844 na Vyama ambavyo havipatikani 2,103.

Kutokana na maagizo hayo, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2019 COASCO ilikagua Vyama vya Ushirika vipatavyo 4,413 sawa na asilimia 102.63 ya lengo la Serikali la kukagua Vyama 4,300.

Katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa, vyama 303 (6.87%) vilipata Hati inayoridhisha, Vyama 2,378 (53.89%) vilipata Hati yenye shaka, Vyama 879 (19.92%) vilipata Hati isiyoridhisha na Vyama 853 (19.32%) vilipata Hati mbaya.

Waziri Hasunga alisema kuwa Kati ya Vyama Vikuu 38, Vyama 4 vilipata Hati Safi, Vyama 22 vilipata Hati yenye shaka, 9 vilipata hati isiyoridhisha na 3 hati mbaya. Vyama hivyo Vikuu 3 vilivyopata HATI MBAYA inayohusisha hoja zenye viashiria vya ubadhirifu wenye Jumla ya shillingi 856,357,955 kwa RUNALI, SCCULT 4,878,662,431 na KYECU kwa kukosekana kwa hati za kuhesabu mali za kudumu mwisho wa mwaka.

 

Alisema kuwa Chama Kilele (Shirikisho-TFC) kimepata Hati Isiyoridhisha ambayo inajumuisha fedha benki zisizofanyiwa malinganisho na pia kutooneshwa katika taarifa za fedha kiasi cha shilling 1,538,726,787

 

Kati ya Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS) 2,710 vilivyokaguliwa, vyama 15 vilipata Hati Safi, 1347 Hati yenye Shaka, 599 Hati Isiyoridhisha na vyama 749 vilipata Hati Mbaya.  Matatizo makuu katika vyama hivyo vya AMCOS ni kushindwa kuandika vitabu vya hesabu, malipo mengi kutokuwa na vielelezo vya malipo, mifumo dhaifu ya udhibiti wa makusanyo na mauzo ya mazao, kukosekana kwa daftari la mali za vyama na watendaji wa vyama kutokuwa na weledi wa kuandika vitabu na taarifa za fedha za vyama. Kati ya SACCOS 1,448 SACCOS 261 zilipata Hati Safi, 887 yenye Shaka, 218 Isiyoridhisha na 82 Hati Mbaya.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyataja matatizo makuu ya SACCOS nyingi kuwa ni kushindwa kuandika vitabu ipasavyo, marejesho ya mikopo ya wanachama kutofanyika kwa wakati, baadhi ya waajiri kuchelewesha kuwasilisha makato ya wanachama kwa SACCOS, madeni makubwa yanayothiri utendaji wa SACCOS, miamala ya benki kutofanyiwa malinganisho na baadhi ya miamala kuwa na ubadhirifu.

Mhe. Hasunga amesema kuwa katika ukaguzi wa kawaida kwa mwaka 2018/2019 fedha zenye mashaka (nia ovu) ni shilingi bilioni 87.6 Hasara iliyotengenzwa kwa uzembe ni shilingi Bilioni 22. 8 huku Wizi/Ubadhirifu ikiwa ni shilingi Bilioni 2.8 ambapo jumla ya fedha hizo ni Bilioni 113.3.

Waziri Hasunga ameongeza kuwa katika ukaguzi maalum kwa mwaka huo wa 2018/2019 fedha zenye mashaka (nia ovu) ni Bilioni 6.2 Hasara iliyotengenzwa kwa uzembe ni Bilioni 2.6 wakati Wizi/Ubadhirifu ni Bilioni 1.7 ambapo jumla ni Bilioni 10.6.

 

Mhe. Hasunga ameongeza kuwa jumla kuu ya fedha za ukaguzi wa kawaida na ukaguzi maalumu ni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mi Tsh 124.

Alisema kuwa mbali na Vyama hivyo vilivyokaguliwa, vipo Vyama 682 vilikataa kuwasilisha vitabu kwa ajili ya ukaguzi na kuongeza kuwa Kati ya vyama 853 vyenye Hati Mbaya, vipo vyama vyenye viashiria vya ubadhirifu wa fedha na mali vipatavyo 130 na vyama vyenye matatizo mbalimbali ya uongozi na utendaji 723.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyoikabidhi TAKUKURU baadhi ya Waajiri wameonekana kuchelewesha michango ya Wanachama baada ya makato na kuathiri uhai wa vyama katika kutoa mikopo kwa Wanachama.