Skip to main content
Habari na Matukio

Waziri Hasunga akutana na AGRI Connect

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga leo amekutana na  wajumbe kutoka Umoja wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya hapa nchini wakiwa wameongozana na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango lengo likiwa ni kupitia na kukubaliana  maeneo ya Utekelezaji wa Mradi kwenye Sekta ya Kilimo unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo wa Umoja wa Jumuiya ya nchi hizo (European union Development fund ) kupitia progamu ya AGRI Connect supporting value chains for shared prosperity .

Wakiongea katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi ya Waziri,walimueleza Mhe. Hasunga kwamba mradi huo wa Agri Connect utakuwa ukitekelezwa kwa  muda wa miaka minne kuanzia  2020-2023  ambapo utagharimu  EURO Millioni mia moja (100) .

Aidha Mradi wa Agri Connect utashughulikia mazao matatu ambayo ni  Kahawa, Chai, na mbogamboga (horticulture ) na vikolezo na kwa upande wa Zanzibar watashughulikia suala la kuongeza mnyororo wa  thamani, kuwajengea uwezo wadau na wakulima na kuboresha masuala ya lishe.

Hata hivyo wamesema maeneo ya  mradi  ni Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe na Katavi wakati kwa upande wa Zanzibar  ni Unguja na Pemba.

Awali wakitoa taarifa yao kwa Waziri wa kilimo Timu hiyo imesema kwamba mradi wa Agri Connect utatekelezwa na makampuni matano ambayo yalishinda zabuni ambapo yatawajengea uwezo wakulima zaidi ya 10,000  wa maeneo ya mradi.

Wamebainisha kwamba mradi huo utagharimu kiasi cha EURO 52millioni na kiasi cha EURO 48Milioni zitatumiwa na wakala wa barabara TARURA kwa ajili ya kujenga miundombinu  ya barabara katika maeneo ya mradi ili kufanikisha  mnyororo wa kuongeza  thamani kwa mazao hayo

Mhe Waziri aliwashukuru na kuwaeleza kwamba mradi huo ulenge Zaidi  kwenye kuhamisha na kuimarisha tecknolojia za uzalishaji na masoko ya bidhaa za wakulima kwa kila zao  ambapo kampuni moja kati hayo lishughulikie mazao ya mbogamboga ,viungo na vikolezo .

Mwisho.