Skip to main content
Habari na Matukio

Wiazara Yasaini Mkataba wa Kuinua Zao la Chai

Wizara wa Kilimo Chakula na Ushirika  na Kampuni ya  Univeler wametia saini ya makubaliano  ya kuanzisha ushirikiano wenye nia ya kufufua na kuendeleza tasnia ya chai hapa nchini.

Kwa mujibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika   Mhe. Eng . Cristopher Chiza ndani ya mkataba huo wakulima wadogo wa chai watanufaika kutokana na makubaliano hayo ambapo hekta 6,000 za mashamba ya chai  zinazomilikiwa na wakulima wadogo zitaboreshwa na kuongeza thamani  kwenye mauzo ya chai kwa zaidi ya thamani ya  Euro milioni 70  kwa mwaka.

Kupitia ushirikiano huu pia ajira zipatazo  5,000 zinatarajiwa kupatikana kwa wananchi wa Tanzania, aliongeza Mhe. Eng .Chiza “Kampuni ya Unilever itafanya kazi na wadau wote  wa tasnia ya chai hapa nchini ambao ni Serikali,Bodi ya Chai Tanzania na wakala waya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania kwa kushirikiana  wadau wengine katika Sekta za umma,  binafsi pamoja na wahisani”, alifahamisha Mhe. Eng .  Chiza Mhe. Eng. Chiza alisema ubia huu unahusisha uwekezezaji katika maeneo ya mashamba yanayomilikiwa na kampuni ya Unilever na mnyororo wa thamani wa zao la chai unaoihusisha kampuni hiyo,ujenzi wa viwanda na miundo mbinu mipya katika maeneo ya uzalishaji,utafiti na maendeleo na program za kuwasaidia wakulima wadogo wa chai.

Ushirikiano huu utatekelezwa kupitia na kufadhiliwa na Mpango wa SAGCOT kama sehemu ya utekelezwaji wa Mpango wa Mageuzi katika Kilimo kupitia azma ya Kilimo Kwanza.

“Makubaliano haya yanaashiria dhamira ya Serikali ya Tanzania katika kutekeleza  azma ya kilimo Kwanza kwa lengo la kukifanya kilimo cha chai kuwa cha kibiashara kwa kuongeza fursa za kipato kwa wakulima wadogo na kusimamia vizuri matumizi ya rasilimali zetu za asili zilizopo” alifafanua Mhe.Chiza.  

Randama ya ushirikiano huu imetiwa saini mjini Dodoma na  Naibu Katibu Mkuu Eng. Mbogo Futakamba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika na Afisa Mkuu Ugavi Kampuni ya Unilever Bwana Pier Luigi Sigismondi.