WIZARA YA KILIMO NA TAHA ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KATIKA KUNDELEZA SEKTA YA KILIMO CHA MBOGA, MATUNDA NA VIUNGO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bwana Andrew Massawe pamoja na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maendelo ya Tasnia ya Mazao ya mboga, matunda na Viuongo Tanzania Horticulture Association (TAHA) Dkt. Jacquiline Mkindi, leo tarahe 22 April, 2022 katika ofisi za Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma, wametia saini makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza Sekta ndogo ya Kilimo cha matunda na mboga (Horticulture) nchini.
Akiongea katika hafla hiyo Katibu Mkuu Massawe amesema Wizara ya Kilimo na Taasisi ya TAHA wameingia makubaliano hayo ili kuendelea kushirikiana ambapo maeneo yafuatayo yataenda kupewa kipaumbele;
Kukuza mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara; Kubadilishana teknolojia ili kukuza tija katika uzalishaji; Utafiti na uendelezaji wa Sekta ndogo ya mboga, matunda na viungo (Horticulture).
Eneo linguine ni pamoja na upatikana ji wa masoko ya mazao ya (Horticulture) pamoja na kuendeleza na kuvutia sekta binafsi ili kuendela kuwekeza zaidi.
Katibu Mkuu amesema eneo la upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati pamoja na mambo mbalimbali yanayoihusu sekta hiyo kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na Wadau wa Sekta ya Mazao ya mboga, matunda na viungo.