Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiongea na watumishi wa TARI Uyole

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( wa kwanza kulia) akiongea na watumishi wa TARI Uyole alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo ambalo taasisi ya Stawisha ilikuwa ikiendesha shughuli za uzalishaji mazao ya ngano, viazi mviringo, maharage na mahindi kinyume na mkataba wa makubalino na wizara ya kilimo hali iliyomfanya Katibu Mkuu huyo kuagiza taasisi hiyo isitishe kazi zake ndani eneo la serikali. Agizo hilo limetekelezwa na Stawisha wamefunga ofisi hizo.