WAZIRI WA KILIMO PROF.ADOLF MKENDA AKISISITIZA JAMBO

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ameiagiza Bodi ya Wakala wa Mbolea wa Taifa TFRA kuhakikisha kuwa mbolea inapatikana kwa gharama nafuu kwa wakulima na inapatikana kwa wakati ili kumsaidia mkulima mdogo aweze kupata tija katika kilimo chake

Prof. Mkenda ametoa maagizo hayo hivi karibuni katika ukumbi wa LAPF aliopo Dodoma mjini huku akiongeza kwamba mapinduzi ya kilimo yatapatikana endapo wakulima watatumia mbolea kulingana na maelekezo ya maafisa ugani.

Mheshimiwa Waziri ameitaka Bodi hiyo kuongea na waagizaji pamoja na taasisi nyingine zinazohusika ili kuhakikisha kwamba bei ya mbolea inabaki kama iliyotumika mwaka jana na kuhakikisha kwamba inawafikia wakulima kwa wakati.

Waziri huyo amebainisha kwamba tatizo lililopo katika sekta ya kilimo ni tija ndogo ambayo inasababishwa na mambo mengi likiwemo la  kutotumia mbolea ipasavyo na idadi  ndogo ya mimea katika ekari (Plant population)