KM Apokea Vitabu vya ASDP II Kutoka Bill and Melinda Gates na USAD
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Eng. Mathew Mtigumwe amepokea jumla ya vitabu na majarida 1600 kutoka kwa mshauri mwelekezi wa mfuko wa Bill and Melinda Gates foundation Professor Marcelina Chijoriga walipokutana ofsini kwake hivi karibuni
Akiongea na KM Professor Chijoriga amesema kuwa taasis ya Bill and Melinda Gate imegawa vitabu vikubwa vya kingereza 500, vitabu vidogo vya kiswahili 400 vitabu vidogo vya kingereza 100 na vipeperushi 900 ili viweze kutumika wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili ASDP II.
Naye KM ameishukuru taasis hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa michango yao kwa lengo la kuendeleza sekta ya kilimo
Pamoja na Bill and Melinda Gate tumepokea vitabu vingine 200 kutoka shirika la USAD lengo likiwa ni kufanikisha uzinduzi wa programu hiyo ya kuendeleza sekta kilimo wawamu ya pili utakao fanyika hivi karibuni
Aidha vitabu hivyo vinauelezea mradi huo wa ASDP II kwa namna ambavyo utatekelezwa, vipaumbele vyake pamoja na namna ya ushirikishwaji wa sekta za kilimo na sekta binafsi