Skip to main content
News and Events

MPANGO MKAKATI WA KUENDELEZA ZAO LA MPUNGA WAZINDULIWA

Mpango Mkakati wa kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga awamu ya pili kutoka tani milioni 28 hadi tani milioni 56 ifikapo mwaka 2030 kwa nchi wanachama (National Rice Development Strategy Phase II - NRDS II) umezinduliwa rasmi leo katika Ukumbi wa Edema ulioko Msamvu Morogoro mjini. Akiongea wakati wa uzinduzi huo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtingumwe amesema kwamba Mpango huo mkakati wa kuendeleza zao la Mpunga Utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi na miwili (12) kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2030. Amesema kwamba mchakato huo umetokana na umoja wa wadau wa maendeleo wa uendelezaji wa zao la mpunga "Coallition for African Rice Development" (CARD), ambapo makao makuu yake yako Nairobi, Kenya. Mhandisi Mtigumwe amesisitiza kwamba Tanzania ni moja kati ya nchi 32 ambazo ni wanachama wa CARD "Coallition for African Rice Development" ambayo ina wabia 23 wakiwemo JICA, Benki Kuu ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika . “Ongezeko la uzalishaji wa mpunga katika nchi ya Tanzania unategemewa kuongeza kuaniz tani milioni (2) kwa sasa hadi kufikia tani milioni (4) mwaka 2030” alisema Mhandisi Mtigumwe Hata hivyo Mhandisi Mtigumwe amewashukuru waandaaji wa kikao hicho hususani Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na HELVETAS ambao wamekuwa nguzo kubwa katika kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo hapa nchini. Amewataka wadau hao kudumisha mashirikiano hayo na Wizara ya Kilimo kwa kuwa ni miongoni mwa sekta muhimu katika kufanikisha maendeleo ya uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla. Matarajio ya mkakati huo unalenga kuongeza uzalishaji mara mbili zaidi, kutoka tani 2,219,628 kwa mwaka 2018 za sasa na kufikia tani 4,500,000 ifikapo mwaka 2030 alisistiza hayo Mhandisi Mtingumwe. Awali akimkaribisha mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japani (JAICA) Bwana Suzuki- san , Mkurugezi wa Idara ya Zana za Kilimo na Umwagiliaji Mhandisi Joseph Lubilo alifafanua kwamba CARD ilianzishwa mwaka 2008 ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji kutoka tani milioni 14 hadi tani milioni 28 ifikapo 2018 kwa nchi wanachama, wakisaidiwa na Steering Committee members (SC) Amesema kwamba wadau na wabia wa maendeleo walipo chini ya CARD ni AfDB, Africa Rice Center, AGRA, FAO, FARA, IFAD, IRRI, JICA, JIRCA, NEPAD, na Benki ya Dunia. Mhandisi Lubilo aliendelea kusema kwamba nchi wanachama zilizonufaika na mpango huo ni Cameroon, Ghana, Guinea, Kenya, Madagascar, Mali, Msumbiji, Nigeria, Senegal, SierraLeone, Uganda, Bennin, Burkina Faso, Code D`Ivoire, CAR, DR Congo, Ethiopia, The Gambia, Liberia, Rwanda, Togo, Zambia na Tanzania. Naye mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) Bwana Suzuki- san amesema zao la mpunga ni muhimu katika Taifa la Tanzania kwa kuwa ndilo linalotumiwa zaidi na wanachi ukiondoa mahindi. Amesema kwamba takwimu za shirika la chakula duniani limeonesha kwamba kwa mwaka 2018 Tanznaia ilizaisha zaidi ya tani milioni tatu (3) za mpunga kutokana na uwezo wa zao hilo kustawi na kukubalika kwa wakulima. Mwisho