PROF.ADOLF MKENDA AKIONGEA NA KIONGOZI WA GEREZA LA KWITANGA ALIPOTEMBELEA VITALU VYA MICHIKICHI

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda hivi karibuni ametembelea vitalu vya miche ya michikichi katika shamba linalomilikiwa na gereza la Kwitanga lililopo Mkoani Kigoma.

Prof Mkenda ameitaka Taasisi hiyo ambayo inashirikiana kwa ukaribu na Taasis ya Utafiti wa kilimo TARI kuhakikisha miche inapatikana kwa wingi ili wakulima wazipate kwa urahisi lengo likiwa ni kuongeza uwezo wa kuzalisha  mafuta ya kupikia .

Serikali inatumia kiasi kikubwa cha fedha  kuagiza mafuta ya kupikia kutoka  nje ya Nchi ambayo yangeweza kuzalishwa hapa nchini  hivyo ni jukumu la TARI kuhakikisha kwamba taifa linajitosheleza kwa bidhaa hiyo hapa nchini, alisisitiza Prof. Mkenda.