Skip to main content
News and Events

Sekta ya Fedha yatakiwa kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Kilimo

Na Bashiri  Salum, Wizara ya Kilimo

Dodoma.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe leo (tarehe 7 Novemba 2019 )ameeleza umuhimu wa taasisi za kifedha kuongeza uwekezaji katika Kilimo na kupunguza masharti ili mkulima aweze kukopa Zaidi

Amesema Kilimo hakitakuwa kwa haraka kama inavyotegemewa na serikali haitaweza kufikia malengo endapo uwekezaji  katika sekta ya Kilimo.

Maelezo hayo aliyatoa wakati wa kikao kilichofanyika katika ukumbi wa  ms ekwa ulioko ndani ya ya majengo ya bunge la jamhuri ya muungano amabapo ambapo wadau hao walito mawasilisho mbalimbali juu ya kuongeza uwekezaji katika kilimo.

Aidha mikutano uliwakutanisha wadau wa Sekta ya Kilimo Benki ya Kilimo (TADB) ,Benki ya  CRDB Benki ya,NMB, Kamati ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji,Kamati ya bunge ya bajeti, Shirika la Kilimo Afirika (AGRA),Mtandao wa wakulima wadogo Tanzania (MVIWATA), SAGCOT, na Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo.

Akiongea wakati wa mikutano huo Mhe. Bashe amesema kwamba asilimia mia moja (100%) ya mikopo inayotolewa na benki ni asilimia na netu (8%) zinaelekezwa katika sekta ya Kilimo kiasi ambacho ni kidogo sana kwa kuinua sekta.

Kiwango hicho cha asilimia 8 huelekezwa katika Kilimo asilimia 92 inaenda kwenye sekta ambazo hazihusiki na Kilimo wakati asilimia 75 ya watanzania wanategemea kilimo,zaidi ya asilimia 85 ya chakula hapa nchini kinatokana na kilimo, uwekezaji mkubwa unatakiwa ufanyike ili Kilimo kiendelee kuzalisha malighafi ya viwanda.Alisema Mhe. Bashe

Uwekezaji huo unatakiwa kuanzia shambani mpaka sokoni ili mkulima aweze kuuza mazao yake. Katika kukabiliana na hali hii tumeona ni vyema kukutana na ninyi wadau wetu katika sekta ya Kilimo kuona namna ya kumsaidia mkulima kuweza kupata mkopo kwa ajili ya kilimo.

Aidha Mhe. Bashe amewata ka wadau wa sekta ya fedha waliohudhuria kikao hicho kujadili namna ambavyo wataweza kusaidia Kilimo kiweze kukua  , kwani Kilimo hakiwezi kukua kama hakuna uwekezaji wa kutosha.

Lengo kubwa la kuitisha mikutano huo ni kuonana mna ambavyo sekta ya fedha   itasaidia sekta ya Kilimo katika kutoa mikopo kwa bei nafuu na kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na wanavyotoa kwa sasa, Mhe.Bashe aliendelea kusisitiza.

Akiwasilisha andiko lake katika mikutano huo Mkurugenzi Mkuu wa benki ya Maendeleo ya Kilimo amesema kwamba kabla hatujaanza kufikiria namna ya kuboresha mkopo kwa mkulima, tufikirie kwanza  je huyu mkulima ameandaliwa vipi katika kupata mkopo huo na ameshapata elimu ya kutosha kuhusiana na mkopo?

Hii inaonesha kwamba wakulima wengi hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na   pia kinachofanya mkopo kupungua katika sekta hiyo. Hata hivyo ameendelea kusema kwamba katika zao la tumbaku hawakupata shida kwani kiwango cha mkopo kilichochukuliwa kilirejeshwa kwa

Naye mwenyeki wa kamati ya bunge ya Kilimo maji na mifugo Mahamudi Mgimwa amesema uwekezaji katika Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye uchumi wa viwanda.

“Hatuwezi kufanikiwa kwenye sekta ya Kilimo kama hatujawekeza vizuri kwenye Kilimo ambacho kinahitaji mitaji mikubwa”alisema Mhe. Mgimwa.

Hata hivyo Mhe. Mgimwa amesisitiza taasisi za benk kupunguza makato kwa wakulima na kuwashauri kuongeza mitandao wa kibenki ili iweze kuwafikia wakulima wote nchini.

Mwanyekiti huyo ameikumbusha sekta binafsi kutumia fursa ya kuwekeza kwenye Kilimo hasa katika wakati huu ambao serikali imepunguza bajeti kwenye sekta ya kilimo.

Akiongea wakati wa wasilisho lake Prof David Nyange mshauri wa mambo ya Sera toka wizara ya Kilimo amesema kwamba sekta ya Kilimo imeendelea kukua kwa asilimia tatu (3%)  hivyo kufanya ukuaji wa maskini kukuwa kwa wastani

Amesema kuna umuhimu wa kuwekeza kwenye  sekta ya Kilimo na kwenye sekta ya viwanda hasa viwanda vya uchakataji wa mazao ya Kilimo ili kuweza kushusha kasi ya ukuaji wa umaskini.

Pof ameongeza kwamba kasi ya ukuaji wa usalama wa chakula imekuwa kubwa hivyo kupunga kazi ya ukuaji wa kasi ya utapiamlo,

Utapiamlo umekuwa ukishuka kwa slimia 1% kwa mwaka wa kati umaskini umekuwa ukishuka kwa 0.5% kwa mwaka hivyo itachukua miaka 30 kuondoa utapiamlo hapa nchini na miaka 50 kuondoa umaskini hapa nchini kama uwekezaji hautafanyika kwenye sekta ya kilimo, alisema Prof. Nyangi.