MKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAZAO BAADA YA KUVUNA

Uzalishaji wa chakula nchini Tanzania, unatosheleza mahitaji ya taifa. Hata
hivyo, baadhi ya mikoa huathirika kwa uhaba wa chakula kutokana na
mifumo hafifu ya kuhifadhi mazao baada ya kuvuna, hali inayosababisha
upungufu wa mazao na kupanda kwa bei. Hali hiyo inatokana na upotevu
wa mazao baada ya kuvuna unaokadiriwa kuwa kati ya asilimia 30 na 40
kwa mazao ya nafaka na asilimia kubwa zaidi kwa mazao yanayoharibika
haraka. Hali ya upotevu wa mazao baada ya kuvuna nchini imeifanya
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuandaa Mkakati wa Taifa
wa Usimamizi Mazao baada ya Kuvuna. Mkakati huu utatekelezwa
kwa kipindi cha miaka kumi na utahusisha mazao ya aina mbalimbali
yakiwemo mazao ya nafaka, jamii ya mikunde, matunda, mboga, mizizi
pamoja na mazao ya mbegu za mafuta. Aidha, mkakati umeainisha
afua mkakati zitakazowezesha kupunguza upotevu wa mazao baada ya
kuvuna na hatimae kuimarisha usalama wa chakula na lishe hapa nchini.
Kudhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvuna kutasaidia jamii kuwa
na uhakika wa chakula na lishe bora na kuongeza kipato bila kutumia
rasilimali za ziada.
Inatambulika duniani kote kuwa kudhibiti upotevu wa mazao unaotokea
wakati wa kuvuna mpaka chakula kinapofika mezani kunatoa fursa kubwa
ya kupunguza baa la njaa na kuchochea ukuaji wa viwanda. Hivyo, juhudi
zinapaswa zielekezwe kwenye uzalishaji wa mazao kulingana na mahitaji
pamoja na kuongeza thamani na matumizi ya bidhaa za mazao.
Mkakati huu unalenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo wadau wa
usimamizi wa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna kwa
lengo la kuongeza kipato na uhakika wa chakula na lishe. Aidha, mkakati
utachangia kutekeleza Sera ya Taifa ya Kilimo, inayotekelezwa kupitia
Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili. Program hii
inalenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo, ili kuongeza uzalishaji na
tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima
wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha yao, uhakika wa usalama
wa chakula na lishe, kuongeza upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya
maendeleo ya viwanda na kuchangia pato la taifa. Pia, mkakati

 

 

PAKUA HAPA

Download File/s: