MKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAZAO BAADA YA KUVUNA KWA LUGHA NYEPESI

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo
wataalam kutoka Serikalini, wasomi wa vyuo vikuu, jukwaa la
Wadau wa usimamizi wa mazao baada ya kuvuna, asasi zisizokuwa
za kiserikali na mashirika ya kimataifa yanayojishughulisha na
kilimo, imeandaa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao Baada
ya Kuvuna katika Lugha Rahisi.
Matumaini ya wizara ni kuwa, uandaaji na utekelezaji wa mkakati
huu utapunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuchangia
ipasavyo katika kuimarisha uhakika na usalama wa chakula na lishe
nchini. Pia, mkakati huu utachangia kuongeza kipato cha mkulima na
Taifa kwa ujumla.
Wizara inapenda kukishukuru kikosi kazi kilichojumuisha wataalam
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Viwanda
na Biashara, Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF)
na Shirika la HELVETAS Swiss Intercooperation kwa kuandaa
mkakati huu. Aidha, Wizara inatoa shukrani za pekee kwa Shirika
la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC), Umoja wa Mapinduzi
ya Kijani Afrika (AGRA), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja
wa Mataifa (FAO) na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na maswala ya
kijamii (ESRF) kwa msaada wao mkubwa wa kifedha, kitaalamu na
kiufundi katika uandaaji wa mkakati huu.

 

Pakua Hapa

Download File/s: