Skip to main content
Habari na Matukio

KITUO CHA UMAHIRI KITAONGEZA VIRUTUBISHO KWENYE NAFAKA

Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema Kituo cha Umahiri cha Uhifadhi wa Nafaka kilichopo Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma pamoja na majukumu mengine kitatumika kuandaa nafaka zilizoongezwa virutubisho.

Waziri Bashe amesema hayo tarehe 20 Agosti 2024 wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo hicho ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Philip Mpango.

"Mhe. Makamu wa Rais leo umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo hiki cha kudhibiti uharibifu wa mazao baada ya kuvunwa, katika kituo hiki tani  62 za unga zitachakatwa hapa na uwekaji wa virutubisho kwenye unga.  Hivyo, hatutahitaji nafaka zilizoongezwa virutibisho kutoka nje ya nchii,” amesema Mhe. Waziri Bashe.

Aidha, Waziri Bashe ameongeza kuwa katika eneo la mradi huo kutakuwa na kituo jumuishi cha zana za kilimo zikazowawezesha wakulima kukodi zana za kisasa za kilimo kwa bei nafuu.

Mradi wa Kituo cha Umahiri cha Uhifadhi wa Nafaka unatekelezwa na Wizara ya Kilimo kupitia Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC).