RAIS SAMIA AKISAFISHA KAHAWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika kichanja (dryer) cha kusafisha na kuanika Kahawa aina ya Arabica ya Kampuni ya AVIV Tanzania Limited tarehe 24 Septemba 2024 wakati wa ziara yake katika Shamba la kampuni hiyo.
Zoezi hilo ni kwa ajili ya usindikaji wa Kahawa ili kupata muonjo bora ambao ndiyo unamuwezesha mkulima kupata bei nzuri sokoni.