TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA 83 WA ICAC 2025
Tanzania imependekezwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Ushauri wa Zao la Pamba Duniani (International Cotton Advisory Committee - ICAC), Novemba 2025.
Pendekezo hilo limekuja kufuatia ushiriki wa Tanzania kama mwanancha, ambapo ujumbe wake unaoongozwa na Dkt. Hussein Mohamed Omar, Naibu Katibu wa Wizara ya Kilimo (anayeshughulikia Maendeleo ya Mazao) katika Kikao cha 82 kinachofanyika katika jiji la Tashkent, nchini Uzbekistan.
Dkt. Omar pia alipata wasaa wa kushiriki katika majadiliano yaliyoshirikisha pia Waziri wa Kilimo wa Uzbekistan, Mhe. Dkt Ibrahim, Katibu Mkuu wa ICAC, Dkt Erick na Mwenyekiti Bw. Lalit K. Gupta wa ICAC kutoka India.
Washiriki wengine kutoka Tanzania ni Dkt. Saidia, Mkurugenzi wa TARI - Ukiriguru na Bw. Marco Mtunga, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi wa Pamba.