Maghala ya Kuhifadhi Chakula
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa maghala 28 ya kuhifadhi nafaka katika eneo la ghala la Luhimba, Mkoani Ruvuma leo tarehe 24 Septemba 2024 ambayo yanaenda kuwa mkombozi kwa wakulima.