WAKULIMA WA PAMBA WAAHIDIWA NEEMA
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara ya Kilimo itaendelea kuboresha maslahi ya wakulima wa pamba kwa kutafuta masoko yenye bei nzuri na kuvutia wawekezaji wa viwanda vitakavyotumia malighafi zitokanazo na zao hilo.
Amesema hayo tarehe 5 Oktoba 2024 kwenye kilele cha Tamasha la Pamba la Simiyu lililopewa jina la “Simiyu Pamba Festival”, kwenye viwanja vya Lagangabilili, Wilaya ya Itilima, Mkoani Simiyu.
Aidha, Naibu Waziri Silinde ameiagiza sekretarieti ya mkoa wa Simiyu kuweka maadhimisho ya tamasha hilo kwenye mipango yao ya kila mwaka kwani litawanufaisha wakulima kwa kupata fursa ya kujifunza mambo muhimu yanayohusiana na uzalishaji wa pamba na mazao mengine.
Mhe. Silinde pia amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Kenani Kihongosi na viongozi wote wa Mkoa huo kwa ushirikiano na ubunifu mkubwa wa tamasha hii ambalo wakulima wamepata fursa ya kupata maarifa ya kilimo cha pamba.