Hali ya Chakula nchini kuelekea mwaka 2017
Hali ya chakula mwaka 2016/2017 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016. Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) ya uzalishaji wa mazao ya chakula iliyofanyika mwezi Julai 2016, nchi inajitosheleza kwa chakula kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 123. Kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara
Hali ya chakula nchini kuelekea mwaka 2017
1. Hali ya Chakula
Hali ya chakula mwaka 2016/2017 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016. Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) ya uzalishaji wa mazao ya chakula iliyofanyika mwezi Julai 2016, nchi inajitosheleza kwa chakula kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 123. Kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara Mikoa 11 ilibainika kuwa na viwango vya ziada vya chakula mikoa 12 ina hali ya utoshelevu na mikoa 2 ina uhaba wa chakula. Katika mikoa 15 ilibainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika Halmashauri 43 hatahivyo mkoa wa Kagera na lamashauri 3 za mkoa huo zimekuwa na maeneo tete baadaye kutokana na athari za tetemeko la ardhi pamoja na ukame ulioathiri mazao kwa kiasi kikubwa.Kwa ujumla hali ya chakula inaridhisha ukilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuwa kulikuwa na jumla ya Halmashauri 69 zilizokuwa zimebainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika mwaka uliopita.
2. Uzalishaji wa Chakula
Taarifa ya Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kitaifa, uzalishaji wa chakula utafikia tani 16,172,841 za chakula (kwa mlinganisho wa nafaka – Grain Equivalent), ambapo tani 9,457,108 ni za mazao ya nafaka na tani 6,715,733 ni za mazao yasiyo nafaka. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2016/17, tunahitaji tani 13,159,326 ambapo tani 8,355,767 ni za mazao ya nafaka na tani 4,803,560 ni za mazao yasiyo nafaka.
Uzalishaji wa zao la mahindi katika mwaka 2015/2016 ulikuwa tani 6,148,699 ambapo mahitaji kwa mwaka 2016/2017 ni tani 5,202,415. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 946,284 za mahindi kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 118. Kwa upande wa uzalishaji wa mchele, jumla ya tani 2,229,071 zilizalishwa kwa mwaka 2015/2016 ambapo mahitaji ya zao hilo kwa mwaka 2016/2017 ni tani 976,925. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 1,252,146 za mchele kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 228.
3. Hifadhi ya Chakula ya Taifa
Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 umepanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula. Hadi kufikia tarehe 24 Novemba 2016, Wakala umenunua jumla ya tani 61,145.245 za chakula sawa na asilimia 61 ya lengo ililojiwekea. Kati ya kiasi hicho, tani 38,132.389 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,012.906 kupitia vikundi vya wakulima. Hata hivyo, hadi kufikia tarehe 24 Novemba, 2016 Wakala umetoa jumla ya tani 20,048.521 za chakula. Aidha, hadi kufikia tarehe 26 Disemba, 2016 Wakala una akiba ya tani 90,716.798 za chakula.
4. Matarajio ya Hali ya Chakula
Tanapoanza mwaka 2017, tunatarajia hali ya chakula kuendelea kuwa ya kuridhisha kutokana na mavuno ya msimu uliopita wa 2015/2016. Bei ya chakula husuani mahindi katika kipindi hiki imepanda kidogo ukilinganisha na bei za mwaka jana mwezi kama huu. Mwenendo wa kupanda kwa bei ya mazao unatokana na kupungua kwa uingizaji wa mazao sokoni ambayo ni hali ya kawaida kila mwaka. Bei ya mchele sokoni bado ni ya kuridhisha.
Mvua za vuli zilichelewa kuanza na zimenyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko usioridhisha katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Uzalishaji unaotokana na mvua za vuli huwa unachangia takribani kati ya asilimia 17 hadi 20 ya chakula nchini. Aidha, maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (mvua za msimu) mvua zimeanza pia kwa kuchelewa na za chini ya kiwango. Hali hiyo, kwa kiasi fulani inazidi kuathiri uingizaji mazao ya chakula kwa wingi sokoni na hasa mahindi kutokana na wafanyabiashara kuhodhi mazao hayo wakiwa na mategemeo ya bei kupanda baada ya taarifa za hali ya unyeshaji mvua kuonyesha kuwa mvua zitakuwa chini ya kiwango na hivyo uzalishaji unategemewa kutokuwa wa kuridhisha.Mabadiliko ya tabia nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia mvua kunyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko mbaya.
Wizara inaendelea kuwasiliana na mikoa ili kufuatilia kwa karibu hali ya upatikanaji wa chakula pamoja na bei, mwenendo wa mvua na hali ya mazao mashambani.Taarifa zinazopatikana zitaisaidia Serikali na kuchukua hatua stahiki kulingana na hali itakayojitokeza. Aidha, tathmini ya kina ya hali ya chakula na Lishe inatarajiwa kufanyika katika maeneo yenye hali tete mwanzoni mwa mwezi Januari 2017 ili kubaini idadi ya watu walioathirika na mahitaji ya chakula na mbegu.
5. Ushauri
- Wafanyabiashara watumie fursa ya kuwa na bei nzuri ya mazao kutoa akiba ya mazao waliyoyahifadhikatika maghaliaa yao na kuyaingiza katika soko.
- Wakulimawatumie mvua zinazonyesha kupanda mazao yanastahimili mvua kidogo na yanayokomaa mapema.
- Wataalam wa kilimo wanatakiwa kuendelea kutoa ushauri kwa wakulima juu ya mazao yanayofaa katika maeneo yao ili kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha.
- , Wananchi kote nchini wanatahadharishwa juu ya kuzingatia hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaathiri kwa kiwango kikubwa mzunguko na upatikanaji wa mvua zinazotosheleza uzalishaji wa mazao hapa nchini.
Kiambatisho 1a: Mwenendo wa bei za mazao ya chakula, kwa miaka ya 2002 hadi 2016 | |||||||||||||
(Bei (TSh) kwa Gunia la Kilo 100) | |||||||||||||
MWEZI | |||||||||||||
ZAO | JAN | FEB | MAR | APR | MEI | JUN | JUL | AUG | SEP | OKT | NOV | DEC | |
Mahindi | 2002 | 14,363 | 14,716 | 15,267 | 14,055 | 10,987 | 9,035 | 9,190 | 9,237 | 10,005 | 11,262 | 11,446 | 11,586 |
2003 | 13,471 | 12,413 | 13,028 | 14,089 | 14,333 | 15,025 | 16,347 | 17,215 | 17,323 | 17,713 | 18,678 | 21,804 | |
2004 | 25,260 | 25,957 | 25,816 | 21,154 | 15,855 | 13,400 | 13,997 | 16,069 | 16,239 | 16,440 | 16,652 | 16,467 | |
2005 | 16,221 | 14,298 | 14,656 | 15,500 | 16,020 | 17,072 | 16,839 | 16,372 | 16,402 | 16,364 | 18,763 | 22,099 | |
2006 | 29,945 | 30,594 | 32,046 | 33,139 | 30,406 | 25,973 | 22,112 | 20,554 | 19,679 | 19,460 | 18,789 | 18,095 | |
2007 | 19,104 | 18,283 | 17,815 | 17,026 | 17,371 | 16,882 | 18,241 | 19,528 | 21,802 | 24,394 | 25,468 | 28,281 | |
2008 | 32,065 | 31,181 | 35,458 | 32,798 | 30,090 | 28,194 | 28,628 | 28,867 | 28,792 | 30,927 | 32,391 | 35,029 | |
2009 | 36,612 | 39,314 | 38,022 | 35,959 | 35,005 | 35,245 | 34,128 | 32,481 | 36,801 | 38,439 | 40,930 | 43,841 | |
2010 | 46,111 | 46,472 | 41,426 | 33,864 | 29,542 | 27,530 | 27,745 | 28,259 | 28,988 | 30,217 | 32,050 | 33,695 | |
2011 | 35,133 | 37,531 | 40,740 | 43,666 | 42,265 | 43,326 | 44,524 | 42,246 | 42,227 | 41,492 | 42,242 | 42,976 | |
2012 | 44,437 | 42,388 | 43,270 | 46,751 | 51,185 | 50,378 | 50,165 | 50,487 | 54,291 | 58,120 | 65,498 | 56,318 | |
2013 | 77,416 | 73,192 | 64,842 | 65,431 | 49,096 | 49,967 | 52,554 | 53,539 | 53,686 | 53,826 | 55,674 | ||
2014 | 54,547 | 51,855 | 49,876 | 47,583 | 47,681 | 44,642 | 41,313 | 40,602 | 39,510 | 38,243 | 38,470 | ||
2015 | 38,232 | 37,355 | 39,491 | 47,702 | 47,042 | 48,025 | 52,219 | 56,318 | 57,717 | 57,756 | 63,774 | 65,104 | |
2016 | 67,048 | 67,326 | 63,912 | 57,431 | 55,976 | 53,986 | 57,011 | 55,571 | 56,312 | 63,133 | 72,133 |
Kiambatisho 1b: Mwenendo wa bei ya mahindi