HOTUBA YA MHE. JAPHET HASUNGA (Mb) KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Matokeo ya Tathmini ya Hali ya Chakula nchini yameonesha kuwa Uzalishaji na upatikanaji wa chakula nchini umeendelea kuimarika ukilinganishwa na mahitaji halisi.
Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2018/19 ni tani 16,408,309 na mahitaji ya chakula kwa mwaka 2019/2020 ni tani 13,842,536. Kwa ujumla kuna ziada ya tani 2,565,774. Hali hii inafanya Taifa liwe na kiwango cha utoshelevu wa chakula kwa asilimia 119. Pamoja na hali hiyo, utengamano wa usalama wa chakula unatarajiwa kuwa wa viwango tofauti Kimikoa