MKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAZAO BAADA YA KUVUNA
Uzalishaji wa chakula nchini Tanzania, unatosheleza mahitaji ya taifa. Hata hivyo, baadhi ya mikoa huathirika kwa uhaba wa chakula kutokana na mifumo hafifu ya kuhifadhi mazao baada ya kuvuna, hali inayosababisha upungufu wa mazao na kupanda kwa bei. Hali hiyo inatokana na upotevu wa mazao baada ya kuvuna unaokadiriwa kuwa kati ya asilimia 30 na 40 kwa mazao ya nafaka na asilimia kubwa zaidi kwa mazao yanayoharibika haraka.
Hali ya upotevu wa mazao baada ya kuvuna nchini imeifanya Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuandaa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi Mazao baada ya Kuvuna. Mkakati huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka kumi na utahusisha mazao ya aina mbalimbali yakiwemo mazao ya nafaka, jamii ya mikunde, matunda, mboga, mizizi pamoja na mazao ya mbegu za mafuta. Aidha, mkakati umeainisha afua mkakati zitakazowezesha kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna na hatimae kuimarisha usalama wa chakula na lishe hapa nchini.
Kudhibiti upotevu wa mazao baada ya kuvuna kutasaidia jamii kuwa na uhakika wa chakula na lishe bora na kuongeza kipato bila kutumia rasilimali za ziada.
Inatambulika duniani kote kuwa kudhibiti upotevu wa mazao unaotokea wakati wa kuvuna mpaka chakula kinapofika mezani kunatoa fursa kubwa ya kupunguza baa la njaa na kuchochea ukuaji wa viwanda. Hivyo, juhudi zinapaswa zielekezwe kwenye uzalishaji wa mazao kulingana na mahitaji pamoja na kuongeza thamani na matumizi ya bidhaa za mazao.
Mkakati huu unalenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo wadau wa usimamizi wa kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna kwa lengo la kuongeza kipato na uhakika wa chakula na lishe. Aidha, mkakati utachangia kutekeleza Sera ya Taifa ya Kilimo, inayotekelezwa kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili.
Program hii inalenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo, ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha yao, uhakika wa usalama wa chakula na lishe, kuongeza upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya maendeleo ya viwanda na kuchangia pato la taifa. Pia, mkakati