Skip to main content
Miongozo
Swahili

MWONGOZO WA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA KILIMO

MWONGOZO WA MAFUNZO KWA WAKUFUNZI NA MAOFISA UGANI KATIKA KUFASIRI NA KUTUMIA TAARIFA NA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA KILIMO

Tanzania imeendelea kushuhudia matukio makubwa ya hali mbaya ya hewa kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko haya yamesababisha ongezeko na ukubwa wa majanga yanayohusiana na hali ya hewa ikiwemo mafuriko, ukame, matukio ya upepo mkali na ongezeko la joto. Hivyo kupelekea kupungua kwa maji ya ardhini, ongezeko la wadudu waharibifu na milipuko ya magonjwa. 

Hali hii imeongeza changamoto katika juhudi za kuongeza tija katika sekta ya kilimo na Tanzania inaendeleza juhudi mbalimbali katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na yale ya tabianchi. Juhudi hizi ni pamoja na Mpango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NAPA, 2007); Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012); Mpango wa Taifa wa Kilimo Himilivu (2014-2019), Programu ya Taifa ya Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabianchi (2015-2025); Mwongozo wa Kilimo Kinachozingatia Mabadiliko ya Tabianchi (2017); Taarifa ya Hali ya Nchi na Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya Tabianchi (2017); Mpango wa Taifa wa Pili wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP II 2018) na Mfumo wa Taifa wa Huduma za Tabianchi (2018-2023). Juhudi hizi kwa pamoja zimeonesha dhamira ya serikali, njia na namna ya kushughulika na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi katika sekta ya kilimo. Pamoja na juhudi hizi, bado kuna upungufu katika uelewa wa matumizi sahihi ya taarifa 

Pakua Faili: