PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ASDP II) Novemba, 2017 “
Sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Asilimia 90 ya ardhi ya Tanzania hulimwa na wakulima wadogo. Sekta inatoa ajira kwa asilimia 65.5 na huchangia asilimia 29.1 ya pato la Taifa, asilimia 30 ya soko la nje na asilimia 65 ya malighafi za viwanda.