TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 01-05 Machi, 2021
Wastani wa bei za mahindi, maharage, mtama na viazi mviringo kitaifa zimeshuka kwa asilimia 2, 3, 1 na 3 mtawalia. Bei ya mchele haijabadilika.
Mboga na Matunda (Horticulture): Bei katika masoko mbalimbali nchini zimebadilika kwa viwango tofauti. Bei za nanasi, tango, tikitimaji, pilipili hoho, na kitunguu zimeongezeka kwa asilimia 10, 6, 4, 3 na 2 mtawalia. Bei ya nyanya imepungua kwa asilimia 3.
Kahawa: Hadi kufikia tarehe 04 Machi, 2021 kahawa iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 66,017 zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 130.1
Choroko: Hadi kufikia tarehe 05 Machi, 2021 choroko iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 5,200,367 zenye thamani ya Shilingi bilioni 9.