TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 16-20 Novemba, 2020
Ujumbe Mkuu
Wastani wa bei za mazao makuu ya chakula kitaifa zimeongezeka kwa viwango tofauti ambapo bei za mtama na maharage zimeongezeka kwa asilimia 5 na 2 mtawalia. Bei za mahindi na mchele zimeongezeka kwa asilimia 1 wakati bei za viazi mviringo hazikubadilika.
Korosho: Hadi kufikia tarehe 19 Novemba, 2020 korosho iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 122,613,193 zenye thamani ya shilingi 293,646,045,181. Kwa wiki hili hadi kufikia tarehe 19 Novemba, 2020 kumekuwa na ongezeko la korosho iliyouzwa kiasi cha tani 19,336.680 zenye thamani ya shilingi 47,057,287,758.
Kahawa: Hadi kufikia tarehe 13 Novemba, 2020 kahawa iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 36,830.978 zenye thamani ya Dola za Kimarekani. 74,076,470.19