Skip to main content
Machapisho
Taarifa
Uangalizi na Uthaminishaji
Kiingereza
Swahili

TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 26-30 Oktoba 2020

Wastani wa bei za mazao makuu ya chakula kitaifa zimeongezeka na kupungua kwa viwango tofauti ambapo bei za mtama zimeongezeka kwa asilimia 10 na mchele kwa asilimia 1 na bei za maharage, mahindi, na viazi mviringo zimepungua kwa asilimia 3, 2 na 1 mtawalia.

✓ Mahindi: Bei zimeonekana kuwa za juu zaidi katika soko la Musoma, Dodoma-majengo na Babati. Bei za chini zimeonekana katika soko la Arusha Mjini, Tabora na Mpanda.

✓ Mchele: Bei zimeonekana kuwa za juu zaidi katika soko la Dar es Salaam-Ilala, Dar es Salaam Kinondoni na soko la Babati ambapo bei ya chini imeonekana katika soko la Mpanda na soko la Musoma.

✓ Maharage Bei zimeonekana kuwa za juu zaidi katika soko la Mpanda na soko la Tabora ambapo bei za chini zimeonekana katika soko la Morogoro na Iringa Mjini.

✓ Korosho: Kwa msimu wa 2020/21 wa mauzo, mahitaji mpaka sasa yamezidi korosho iliyopo kwa tani 234,733

Pakua Faili: