Skip to main content
Taarifa
Swahili

TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 3 – 7 Mei, 2021

Wastani wa bei kitaifa zimepungua kwa viwango tofauti tofauti. Bei za mchele, maharage, mahindi, mtama na viazi mviringo zimepungua kwa asilimia 2, 2, 4, 4 na 6 mtawalia.

 Mboga na Matunda (Horticulture): Bei katika masoko mbalimbali nchini zimebadilika kwa viwango tofauti. Bei za nanasi, nyanya na vitunguu zimeongezeka kwa asilimia 8, 4 na 3 mtawalia, wakati bei za tango, pilipili hoho na tikiti maji zimepungua kwa asilimia 22, 16 na 4 mtawalia.

 Kahawa: Hadi kufikia tarehe 7 May, 2021 kahawa iliyouzwa kwa msimu wa mauzo 2020/21 ni tani 69,237 zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 136.3.

 Choroko: Hadi kufikia tarehe 11 Aprili, 2021 choroko zilizouzwa kwa msimu wa mauzo 2021 ni tani 14,112 zenye thamani ya Shilingi bilioni 22.6.

Pakua Faili: