TANGAZO LA KUKARIBISHA MAOMBI YA MASHAMBA YA KULIMA MKONGE
Utangulizi Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) inawatangazia watanzania wote kuwa inatarajia kugawa mashamba kwa ajili ya kilimo cha mkonge kwa wakulima wadogo ili kuendeleza kilimo cha mkonge nchini.
Mashamba yanayokusudiwa kugawiwa kwa wakulima wadogo ni mashamba ya Hale Estate, Magoma Estate, Magunga Estate, Ngombezi Estate na Mwelya Estate yaliyopo Wilaya za Handeni na Korogwe ambayo yanamilikiwa na Bodi ya Mkonge Tanzania ambayo sehemu yalishagawiwa kwa wakulima wadogo.