Skip to main content
Utaratibu wa kuomba vibali vya kusafirisha chakula nje ya nchi
- Mwombaji lazima awe na TIN No.
- Uwe na Leseni ya Biashara ya Mazao ya Kilimo kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.
- Andika Barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, S.L.P. 2182 Dodoma.
- Barua ionyeshe ni zao lipi unataka kusafirisha nje ya nchi, kwa kiasi gani (tani) na utapitisha kwa njia ipi. Mfano Bandari au Mpaka upi.
- KWA MTEJA AMBAYE ANAOMBA KWA MARA YA PILI
- Mwombaji lazima awe na TIN No.
- Leseni ya Mazao ya Biashara.
- Barua kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, S.L.P. 2182.
- Barua ionyeshe ni zao lipi anataka kusafirisha nje ya nchi, kwa kiasi gani (tani) na atapitisha kwa njia ipi. Mfano Bandari au Mpaka upi.
- Ripoti ya kibali alichopewa mara ya wisho (ikimaanisha utekelezaji wake hivyo hutapewa kibali kingine kama haujaleta ripoti, pia ambatisha nakala ya kibali cha awali)
- SIMU OFISINI: 022 – 2865951 – E-mail: dnfs@kilimo.go.tz
- BARUA ZA VIBALI VYA KUSAFIRISHA CHAKULA NJE YA NCHI ZINAPOKELEWA CHUMBA NA.11 JENGO LA KILIMO I