Skip to main content
Machapisho
Miongozo
Taarifa
Swahili

Maboresho ya Kodi, tozo na ada Sekta ya Kilimo.

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA BIASHARA (BLUEPRINT) KATIKA SEKTA YA KILIMO

Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija ya mazao. Katika kutimiza lengo hilo, Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji kwa kupitia Sera na sheria za kilimo. 

Maboresho ya Kodi, Tozo na Ada katika kilimo yamenufaisha wakulima, kwa sababu baadhi ya tozo hizo hutozwa moja kwa moja kwa wakulima hivyo kupunguza mapato yao. Aidha, baadhi ya Kodi na Tozo zinazotozwa kwa wafanyabiashara zimekuwa zikiathiri ushindani wa mazao ya Kilimo kwenye soko kwa kuwa huongeza gharama za ufanyaji biashara. Hali hiyo husababisha wafanyabiashara kurudisha gharama hizo kwa wakulima kwa kupunguza bei za mazao wanazolipa kwa wakulima. 

Serikali katika kipindi cha miaka mitano (5) pamoja na mambo mengine imefanya maboresho ya Kodi, Ada na Tozo mbalimbali katika sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo sekta ya kilimo (mazao). Maboresho hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Programu ya kuendeleza Sekta ya kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) hususan eneo Kuu la Nne linalohusu kuweka mazingira wezeshi ya kuendeleza Sekta ya kilimo na kuwezesha Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini na vilevile utekelezaji wa Mpango wa kuboresha Mfumo wa udhibiti wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business Environment). 

Download here

Pakua Faili: