Nyaraka » Publications

Hali ya Chakula nchini kuelekea mwaka 2017

  • Hifadhi ya Mahindi, Tanzania

Hali ya chakula mwaka 2016/2017 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016. Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) ya uzalishaji wa mazao ya chakula iliyofanyika mwezi Julai 2016, nchi inajitosheleza kwa chakula kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 123. Kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara

Hali ya chakula nchini kuelekea mwaka 2017

1.  Hali ya Chakula

Hali ya chakula mwaka 2016/2017 ni ya kuridhisha kutokana na mavuno yaliyopatikana msimu wa kilimo wa 2015/2016. Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) ya uzalishaji wa mazao ya chakula iliyofanyika mwezi Julai 2016, nchi inajitosheleza kwa chakula kwa viwango vya utoshelevu vya asilimia 123. Kati ya mikoa 26 ya Tanzania Bara Mikoa 11 ilibainika kuwa na viwango vya ziada vya chakula mikoa 12 ina hali ya utoshelevu na mikoa 2 ina uhaba wa chakula.  Katika mikoa 15 ilibainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika Halmashauri 43 hatahivyo mkoa wa Kagera na lamashauri 3 za mkoa huo zimekuwa na maeneo tete baadaye kutokana na athari za tetemeko la ardhi pamoja na ukame ulioathiri mazao kwa kiasi kikubwa.Kwa ujumla hali ya chakula inaridhisha ukilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuwa kulikuwa na jumla ya Halmashauri 69 zilizokuwa zimebainika kuwa na maeneo yenye uhaba wa chakula katika mwaka uliopita.

2. Uzalishaji wa Chakula

Taarifa ya Tathmini ya awali (Preliminary Forecast) na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kitaifa, uzalishaji wa chakula utafikia tani 16,172,841 za chakula (kwa mlinganisho wa nafaka – Grain Equivalent), ambapo tani 9,457,108 ni za mazao ya nafaka na tani 6,715,733 ni za mazao yasiyo nafaka. Mahitaji ya chakula kwa mwaka 2016/17, tunahitaji tani 13,159,326 ambapo tani 8,355,767 ni za mazao ya nafaka na tani 4,803,560 ni za mazao yasiyo nafaka.

Uzalishaji wa zao la mahindi katika mwaka 2015/2016 ulikuwa tani 6,148,699 ambapo mahitaji kwa mwaka 2016/2017 ni tani 5,202,415. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 946,284 za mahindi kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 118. Kwa upande wa uzalishaji wa mchele, jumla ya tani 2,229,071 zilizalishwa kwa mwaka 2015/2016 ambapo mahitaji ya zao hilo kwa mwaka 2016/2017 ni tani 976,925. Hivyo, kulikuwa na ziada ya tani 1,252,146 za mchele kwa kiwango cha utoshelevu wa asilimia 228.

3. Hifadhi ya Chakula ya Taifa

Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa mwaka wa fedha 2016/2017 umepanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula. Hadi kufikia tarehe 24 Novemba 2016, Wakala umenunua jumla ya tani 61,145.245 za chakula sawa na asilimia 61 ya lengo ililojiwekea. Kati ya kiasi hicho, tani 38,132.389 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,012.906 kupitia vikundi vya wakulima. Hata hivyo, hadi kufikia tarehe 24 Novemba, 2016 Wakala umetoa jumla ya tani 20,048.521 za chakula. Aidha, hadi kufikia tarehe 26 Disemba, 2016 Wakala una akiba ya tani 90,716.798 za chakula.

4.  Matarajio ya Hali ya Chakula

Tanapoanza mwaka 2017, tunatarajia hali ya chakula kuendelea kuwa ya kuridhisha kutokana na mavuno ya msimu uliopita wa 2015/2016. Bei ya chakula husuani mahindi katika kipindi hiki imepanda kidogo ukilinganisha na bei za mwaka jana mwezi kama huu. Mwenendo wa kupanda kwa bei ya mazao unatokana na kupungua kwa uingizaji wa mazao sokoni ambayo ni hali ya kawaida kila mwaka. Bei ya mchele sokoni bado ni ya kuridhisha.

Mvua za vuli zilichelewa kuanza  na zimenyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko usioridhisha  katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka. Uzalishaji unaotokana na mvua za vuli huwa unachangia takribani  kati ya asilimia 17 hadi 20 ya chakula nchini. Aidha, maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (mvua za msimu) mvua zimeanza pia kwa kuchelewa na za chini ya kiwango. Hali hiyo, kwa kiasi fulani inazidi kuathiri uingizaji mazao ya chakula kwa wingi  sokoni na hasa mahindi kutokana na wafanyabiashara kuhodhi mazao hayo wakiwa na mategemeo ya bei kupanda baada ya taarifa za hali ya unyeshaji mvua kuonyesha kuwa mvua zitakuwa chini ya kiwango na hivyo uzalishaji unategemewa kutokuwa wa kuridhisha.Mabadiliko ya tabia nchi kwa kiasi kikubwa yamechangia mvua kunyesha chini ya kiwango na kwa mtawanyiko mbaya.

Wizara inaendelea kuwasiliana na mikoa ili kufuatilia  kwa karibu  hali ya upatikanaji wa  chakula pamoja na bei, mwenendo wa mvua na hali ya mazao mashambani.Taarifa  zinazopatikana zitaisaidia  Serikali na kuchukua hatua stahiki  kulingana na hali itakayojitokeza. Aidha, tathmini ya kina ya hali ya chakula na Lishe inatarajiwa kufanyika katika maeneo yenye hali tete mwanzoni mwa mwezi Januari 2017 ili kubaini idadi ya watu walioathirika na mahitaji ya chakula na mbegu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     

5. Ushauri

  • Wafanyabiashara watumie fursa ya kuwa na bei nzuri ya mazao kutoa akiba ya mazao waliyoyahifadhikatika maghaliaa yao na kuyaingiza katika soko.
  • Wakulimawatumie mvua zinazonyesha kupanda mazao yanastahimili mvua kidogo na yanayokomaa mapema.
  • Wataalam wa kilimo wanatakiwa kuendelea kutoa ushauri kwa wakulima juu ya mazao yanayofaa katika maeneo yao ili kutumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha.
  • , Wananchi kote nchini wanatahadharishwa juu ya kuzingatia hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaathiri kwa kiwango kikubwa mzunguko na upatikanaji wa mvua zinazotosheleza uzalishaji wa mazao hapa nchini.

Kiambatisho 1a: Mwenendo wa bei za mazao ya chakula, kwa miaka ya 2002 hadi 2016

      (Bei (TSh) kwa Gunia la Kilo 100)

 

MWEZI

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

ZAO

 

JAN

FEB

MAR

APR

MEI

JUN

 JUL

AUG

SEP

OKT

NOV

DEC

Mahindi

2002

14,363

14,716

15,267

14,055

10,987

9,035

9,190

9,237

10,005

11,262

11,446

11,586

 

2003

13,471

12,413

13,028

14,089

14,333

15,025

16,347

17,215

17,323

17,713

18,678

21,804

 

2004

25,260

25,957

25,816

21,154

15,855

13,400

13,997

16,069

16,239

16,440

16,652

16,467

 

2005

16,221

14,298

14,656

15,500

16,020

17,072

16,839

16,372

16,402

16,364

18,763

22,099

 

2006

29,945

30,594

32,046

33,139

30,406

25,973

22,112

20,554

19,679

19,460

18,789

18,095

 

2007

19,104

18,283

17,815

17,026

17,371

16,882

18,241

19,528

21,802

24,394

25,468

28,281

 

2008

32,065

31,181

35,458

32,798

30,090

28,194

28,628

28,867

28,792

30,927

32,391

35,029

 

2009

36,612

39,314

38,022

35,959

35,005

35,245

34,128

32,481

36,801

38,439

40,930

43,841

 

2010

46,111

46,472

41,426

33,864

29,542

27,530

27,745

28,259

28,988

30,217

32,050

33,695

 

2011

35,133

37,531

40,740

43,666

42,265

43,326

44,524

42,246

42,227

41,492

42,242

42,976

 

2012

44,437

42,388

43,270

46,751

51,185

50,378

50,165

50,487

54,291

58,120

65,498

56,318

 

2013

 

77,416

73,192

64,842

65,431

49,096

49,967

52,554

53,539

53,686

53,826

55,674

 

2014

 

54,547

51,855

49,876

47,583

47,681

44,642

41,313

40,602

39,510

38,243

38,470

 

2015

38,232

37,355

39,491

47,702

47,042

48,025

52,219

56,318

57,717

57,756

63,774

65,104

 

2016

67,048

67,326

63,912

57,431

55,976

53,986

57,011

55,571

56,312

63,133

72,133

 

Kiambatisho 1b: Mwenendo wa bei ya mahindi