Skip to main content
Fomu
Miongozo
Miradi
Swahili

MFUMO WA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YATAKAYOTOKANA NA SHUGHULI ZA MRADI JUNI 2018

Mfumo huu ni wa kushughulikia malalamiko yanayoweza kusababishwa na shughuli za utekelezaji wa mradi kama vile ujenzi au ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji na barabara, pamoja na ujenzi wa maghala. Mfumo huu ni nyenzo muhimu katika kusaidia wakulima/wananchi wanaoweza kuathiriwa na shughuli mbalimbali za mradi. Mfumo ni njia inayowawezesha wakulima kupaza sauti na hisia zao juu ya athari zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi na namna ya kuzishughulikia. Mfumo huu unaweka njia ya wazi katika kutatua malalamiko ili kuzuia migogoro isiyokuwa ya lazima ili kufikia malengo ya mradi.

Kwa ujumla malalamiko yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi yanaweza kuhusiana na: 

 1. Uwezekano wa kuharibiwa mazao shambani;
 2. Uwezekano wa kuharibiwa ardhi ya kilimo kwa muda mfupi;
 3. Mkandarasi kutotimiza wajibu wake;
 4. Kuzuiliwa kwa muda mfupi kuingia kwenye mashamba wakati wa ukarabati au ujenzi;
 5. Usumbufu wa upatikanaji wa maji;
 6. Wakulima kutotoa ushirikiano mzuri kwa mkandarasi; n.k.

Kwa kuyatambua hayo Mradi kwa kushirikiana na wadau umeweka mfumo maalumu wa kuyashughulikia hayo endapo yatajitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

 • Wakulima na wananchi watafahamishwa juu ya mfumo huu;
 • Wakulima wataelekezwa namna ya kuwasilisha malalamiko yao na utaratibu utakotumika kutatua migogoro itayojitokeza kwa wakati;
 • Wizara ya Kilimo, Tawala ya Mkoa pamoja na Halmashauri za Wilaya watasimamia uimarishaji/uanzishwaji wa kamati za kushughulikia malalamiko katika ngazi mbalimbali;
 • Mradi utatumia mfumo ambao utahusisha Kamati ya Usuluhishi wa Migogoro ya Skimu ya Umwagiliaji, Serikali ya Kijiji, Kata na Wilaya, Mkoa na Wizara. Ngazi hizi zote zitahakikisha kuwa haki inatendeka wakati wa kushughulikia malalamiko yatakayojitokeza;
 • Muda wa kushughulikia malalamiko utategemea na aina ya malalamiko yatakayojitokeza lakini si zaidi ya siku 7.
 • Utaratibu wa kurudishia/kukarabati miundombinu ya umma au ya binafsi itakayoharibiwa na shughuli za mradi utafanyika baada ya kupata taarifa ya kwa maandishi kutoka taasisi husika au watu binafsi. Kwa upande wa watu binafsi wenye ndoa itahusisha mke na mme. Endapo mkandarasi hatarudishia miundo mbinu aliyoiathiri wakati wa shughuli za ujenzi ghala na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji na barabara, basi taasisi au mtu binafsi anaweza kukata rufaa kwa mamlaka zinazohusika.

UTARATIBU WA KUSIMAMIA MALALAMIKO

Kamati ya Kijiji/Skimu

Katika kila skimu ya umwagiliaji kutakuwa na kamati ya kushughulikia malalamiko yatakayojitokeza kwenye eneo husika. Kamati hiyo itakutana mara moja kwa wiki endapo malalamiko yatakuwa yamejitokeza. Kamati hiyo itajumuisha wajumbe wafuatao:

 1. Wawakilishi wawili wa wakulima au wananchi watakaoathirika na shughuli/kazi za Mradi (Mwanaume 1 na Mwanamke 1); idadi ya wakulima inaweza kuongezwa kutegemeana na idadi ya wajumbe wengine
 2. Mwenyekiti wa Kijiji, ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;
 3. Katibu wa Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Ardhi ngazi ya Kijiji.
 4. Wajumbe wote wa Kamati ya Usuluhishi wa migogoro ya Umoja wa Umwagiliaji, ambapo Mwenyekiti atakuwa Katibu wa Kamati

Kamati ya Wilaya

Katika ngazi ya Wilaya kamati ya kushughulikia malalamiko itakutana mara mbili kwa mwezi kama kutakuwa na malalamiko yaliyowasilishwa na ambayo hayakupata ufumbuzi ngazi ya kijiji. Kamati itakuwa na wajumbe wafuatao:

 • Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;
 • Mkurugenzi wa Wilaya ambaye atakuwa Katibu wa Kamati ya Wilaya;
 • Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya,
 • Afisa Kilimo wa Wilaya au Mratibu wa Mradi wa Wilaya
 • Afisa Ardhi wa Wilaya
 • Mwakilishi mmoja kutoka kila skimu ya umwagiliaji, hususani Mwenyekiti wa Kamati ya Kijiji (Huyu atashiriki tuu pale atakapohitajika na Kamati ya Wilaya)

Mtendaji Kata atapewa taarifa ya malalamiko yote ambayo yatapelekwa kutoka ngazi ya Kijiji kwenda ngazi ya Wilaya.

Rufaa kwenda Ngazi ya Mkoa, Wizara na Mahakama

Hata hivyo ni mategemeo kuwa malalamiko mengi yatashushughulikiwa na kuishia katika ngazi ya Kijiji. Endapo malalamiko hayatapata ufumbuzi au mlalamikaji hataridhika na maamuzi yaliyotolewa, basi malalamiko yanaweza kupelekwa ngazi ya juu au mlalamikaji anaweza kukata rufaa kutoka ngazi moja kwenda nyingine yaani Kijiji, Wilaya, Mkoa na hatimaye Wizara.

Katika ngazi ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa atashughulikia malalamiko yaliyoletwa kutoka ngazi ya wilaya kwa kutumia mfumo wa kawaida wa serikali uliopo. Malamiko yanaweza kupelekwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo endapo kutahitajika kufanya hivyo. Pale itakaposhindikana kabisa kupata ufumbuzi katika ngazi mbalimbali basi mlalamikaji anaweza kukata rufaa na kupeleka malalamiko katika Mahakama ya Mwanzo kwa hatua zaidi. 

Wajibu wa Mkandarasi

Mkandarasi atawajibika katika kuhakikisha kuwa shughuli za ujenzi wa mradi zinafanyika katika maeneo atakayokabidhiwa bila kuharibu eneo jingine nje ya shughuli za mradi au mashamba ya wakulima. Mkandarasi atawajibika kuhakikisha kuwa anaondoa vifaa vyote vilivyotumika wakati wa ujenzi au ukarabati katika eneo la Mradi.

NJIA MBALIMBALI ZITAKAZOTUMIKA KUWASILISHA MALALAMIKO KWENYE MRADI

 1. Kutumia fomu ya malalamiko ya mradi: Fomu la malalamiko itapatikana pia kwenye tovuti ya wizara ya kilimo www.kilimo.go.tz/erpp ili kila mwenye lalamiko anaweza kupakua fomu hiyo. Fomu hiyo itajazwa na mlalamikaji kisha kutumwa kwa Mratibu wa Mradi kwa kutumia barua pepe (email) au anuani ya posta itakayotolewa. Mratibu wa Mradi baada ya kuipokea ataiwasilisha kwa kamati husika ili ipatiwe ufumbuzi.
 2. Kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwenda namba maalum: Mlalamikaji anaweza kutuma lalamiko lake kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (sms) kwenda kwa viongozi wa mradi kupitia namba ya simu +255 (0) 629 622520 na zile zitakazotolewa na Wilaya.
 3. Kupiga simu: Mlalamikaji anaweza kupiga simu kwenda kwa wahusika wowote wa Mradi kupitia ngazi mbalimbali. Aidha namba maalum ya simu ya kushughulikia ni +255 (0) 629 622520.
 4. Kutumia barua pepe: Mlalamikaji anaweza kutuma lalamiko lake kwa njia ya barua pepe kwa Mratibu wa Mradi kisha kuiwasilisha kwa kamati husika ili ipatiwe ufumbuzi.
 5. Njia ya ana kwa ana: Mlalamikaji anaweza kutoa malalamiko yake katika vikao mbalimbali vya kijiji au kwa kiongozi yeyote anayehusiana na mradi katika ngazi mbalimbali.
 6. Kutumia sanduku la maoni: Mlalamikaji anaweza kutumia sanduku la maoni la mradi ambalo litawekwa katika Ofisi ya Kijiji.

Malalamiko yote yatakayowasilishwa yanatakiwa kuingizwa au kuorodheshwa katika daftari la malalamiko kwa ajili ya ufuatiliaji na kumbukumbu. Katika kutumia mfumo huu haki ya mlalamikaji inabidi izangatiwe. 

Kiambatisho 1:  Fomu ya Malalamiko

 

 

 

TAARIFA ZA MTU ALIYEATHIRIWA NA MRADI

Jina La Ukoo:

 

……………….……………...…

Jina la Kwanza:

 

………………….…….………

Majina mengine:

 

………………………...…               

 

Jinsia:  Me ….………     Ke …….…...

Namba ya simu: ……….……………………

 

Kazi:  ………………………………………………………………………..……………………

Hali ya Ndoa:  

 

Ameoa / Ameolewa…

 

Hajaoa / Hajaolewa…

 

 

Ameachika …

Mjane…

 

 

Wametengana…

 

Jina la Mrithi: …………………………

 

Namba ya simu: ………………….………………

 

Anuani  .…………………………………………………………………………………..……                                                           

 

…………………………………………………………………………………………………

 

Kijiji / Kitongoji: ………………………………………………

MAELEZO YA AINA YA MALALAMIKO

 

 

 

 

 

Sahihi ya Mlalamikaji:……………………………

Tarehe: ………….…………….
KWA MATUMIZI YA OFISI TU
Namba ya Shauri………………………………

 

Tarehe lilipofunguliwa…………………

Jina la aliyeandika: ………………………..…
Namba ya Simu ……….………………

 

Mahali :……………………………………..…

 

 

 

Maoni ya Kamati ya Usuluhishi

 

Wilaya:………………………………………………………………...……………………

 

Umetatuliwa……

Rufaa…..Umefungwa…..

 

Sababu za Rufaa:………………………………………..…………………………………….

 

………………………………………………………………………………………………….

 

Jina na Sahihi ya Afisa …………………..………………………

Tarehe: ………………….
  

 

Ijazwe na Mlamikaji / Muathirika
 

 

 
  
Hakuridhika……

 

Ameridhika…….

 

 

Taarifa iliyotolewa hapo juu ni ya ukweli na sahihi kulingana na uelewa wangu.

 

 

Sahihi ya Mlalamikaji: ……………………………

Tarehe: …………………. 
   
           

 

 

Maoni ya Kamati ya Migogoro

    
         
Umetatuliwa:..  Rufaa:….. Umefungwa.    
          

 

Jina  ……………………...............................................................                                                     Sahihi  …………..……………..…

Tarehe: …………..…..