Skip to main content
Miongozo
Taarifa
Swahili

MKAKATI WA TAIFA WA USIMAMIZI WA MAZAO BAADA YA KUVUNA KWA LUGHA NYEPESI

Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam kutoka Serikalini, wasomi wa vyuo vikuu, jukwaa la
Wadau wa usimamizi wa mazao baada ya kuvuna, asasi zisizokuwa za kiserikali na mashirika ya kimataifa yanayojishughulisha na
kilimo, imeandaa Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Mazao Baada ya Kuvuna katika Lugha Rahisi.

Matumaini ya wizara ni kuwa, uandaaji na utekelezaji wa mkakati huu utapunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna na kuchangia ipasavyo katika kuimarisha uhakika na usalama wa chakula na lishe nchini. Pia, mkakati huu utachangia kuongeza kipato cha mkulima na Taifa kwa ujumla.

Wizara inapenda kukishukuru kikosi kazi kilichojumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Jukwaa Lisilo la Kiserikali la Wadau wa Kilimo (ANSAF) na Shirika la HELVETAS Swiss Intercooperation kwa kuandaa mkakati huu. Aidha, Wizara inatoa shukrani za pekee kwa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC), Umoja wa Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na maswala ya kijamii (ESRF) kwa msaada wao mkubwa wa kifedha, kitaalamu na kiufundi katika uandaaji wa mkakati huu.

Pakua Faili: