Skip to main content
Ripoti
Swahili

RASMU YA MAPENDEKEZO YA KUANZISHA WAKALA WA KUSIMAMIA NA KURATIBU MAONESHO YA KILIMO NCHINI

Wizara ya Kilimo (WK) ina jukumu la kukuza ili kuchangia Pato la Taifa,usalama wa chakula, pato la wananchi na kuondoa umaskini. Ili hayoyafikiwe Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine inawajibu wa kufikisha mbinu na kanuni bora za uzalishaji wa mazao na bidhaa za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi.

Wizara inatumia njia na mbinu mbalimbali kufikisha technolojia bora, maarifa na taarifa za kilimo kwa wadau ili viwasaidiekuongeza uzalishaji na tija. Mbinu zinazotumika ni pamoja na kutoa mafunzo kwa njia ya darasa (vyuoni), shamba darasa, vipindi vya redio na luninga, vijitabu, vipeperushi, mabango, magazeti na kupitia maonesho ya kilimo yajulikanayo kama Nane Nane. Maonesho ya kilimo (Nane Nane) yana uzito wa kipekee kutokana na umuhimu na historia ya kuanzishwa kwake. Katika maonesho hayo wakulima na wadau wengine wanapata fursa ya kuona teknolojia mbalimbali za uzalishaji,usindikaji na masoko pamoja na maarifa na taarifa za kilimo kutoka ndani na nje ya nchi.

HISTORIA YA MAONYESHO YA NANENANE

Maonesho ya Kilimo yamekuwepo tangu kabla ya kupata uhuru ambapo yalifanyika katika ngazi ya Wilaya na Mikoa.   Kwa  mfano “Nyamwezi Agricultural Show” yalifanyika miaka ya 1949 hadi miaka ya 1950 katika mikoa ya Kanda ya ziwa (Mwanza, Tabora na Shinyanga)  ambapo wakulima na wafugaji walionesha bidhaa zao. Baada ya uhuru mwaka 1961 Maonesho ya Kilimo na Sherehe za Wakulima ziliendelea kuwepo na baadae kujulikana kama Maonesho ya Sabasaba.

Katika kipindi cha maonesho ya kilimo (sabasaba) mapungufu mengi yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kushindwa kufikisha teknolojia mbalimbali za kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima na wadau wengine ipasavyo.. Maonesho yalikuwa na sura ya kutoa zawadi tu kwa washindi bora wa Vijiji, Wilaya, Taasisi na Mashirika ya umma kinyume na matarajio ya Serikali ya kutoa elimu kwa wakulimakuhusu mbinu bora za kilimo.kutokana na mapungufu hayo, tarehe 20 Oktoba 1992 Wizara ya Kilimo iliitisha Kikao mjini Arusha ambapo iliridhiwa kuanzisha Chama cha Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Society Organisation -TASO) chombo mahsusi cha kuratibu maonesho ya Kilimo

Kwa Taarifa zaidi pakua hapa

Pakua Faili: