Skip to main content
Taarifa
Swahili

TAARIFA YA WIKI YA MWENENDO WA BEI ZA MAZAO YA CHAKULA 24 - 28 Mei, 2021

Wastani wa bei kitaifa umebadilika kwa viwango tofauti.. Bei za mtama na viazi mviringo zimeongezeka kwa asilimia 1 mtawalia, wakati bei za mahindi na maharage hazijabadilika na bei ya mchele imepungua kwa asilimia 1.

Mboga na Matunda (Horticulture): Bei katika masoko mbalimbali nchini zimebadilika kwa viwango tofauti. Bei za nanasi, na vitunguu zimeongezeka kwa asilimia 1, wakati bei za tikiti maji, pilipili hoho na tango, zimepungua kwa asilimia 5, 3 na 2 mtawalia.. 

Pakua Faili: