JAMHURI YA BELARUS YAONESHA UTAYARI KUWEKEZA SEKTA YA KILIMO
Jamhuri ya Belarus yaonesha utayari wa kuwekeza katika Sekta ya Kilimo nchini kufuatia mazungumzo ya pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Belarus, Mhe. Viktor Karankevich, tarehe 3 Juni 2026.
Viongozi nao wamejadili namna ya kuimarisha mashirikiano kati ya Belarus na Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya kutengeneza matrekta na zana zake, miundombinu ya uhifadhi wa mazao, mitambo ya ujenzi wa barabara na kusafisha mashamba pamoja na mashine za kuchakata mazao ili kuongeza thamani.
Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu Mweli ametumia nafasi hiyo kumuomba Mhe. Naibu Waziri Mkuu Viktor Karankevich kuhamasisha kampuni za Belarus kuja kuwekeza Tanzania kwa kuleta teknolojia mbalimbali za kilimo ili wakulima waweze kuzalisha kwa tija na kuongeza kipato.
Katibu Mkuu Mweli amemwakilisha Mhe. Daniel Chongolo (Mb), Waziri wa Kilimo katika ziara ya kikazi nchini Belarus.