Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango akifurahia na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi la ujenzi wa shamba la pamoja la Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Programu ya BBT Mlazo- Ndogowe. tarehe 22 Agosti, 2024
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli akizungumza na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Giuseppe Sean Coppola kuhusu kuimarisha ushirikiano katika Sekta ya Kilimo hususan katika masuala ya utafiti ili kuchochea ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kwenye Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akipokea kwa niaba ya wakulima wa Tumbaku kutoka Tabora na Mikoa mingine ya Kanda ya Kati na Magharibi hundi ya Shilingi Bilioni 1.1 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya wakulima 2,226 kutoka AMCOS 22 ambao mazao yao yaliathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo mvua kubwa na mvua za mawe.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo (Ushirika na Umwagiliaji), Dkt. Suleiman Serera akishiriki katika Mkutano Mkuu wa 56 wa Chama cha Ushirika TANESCO SACCOS Novemba 9, 2024 Jijini Dodoma.
Watalaamu wa afya ya udongo wakiendelea na zoezi la upimaji wa afya ya udongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo ikiwemo chakula, biashara pamoja na mazao ya bustani.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la World Food Programme (WFP) nchini Tanzania, Bw. Ronald Tran Ba Huy tarehe 6 Novemba, 2024 katika ziara yake ya kujitambulisha kwa Waziri wa Kilimo, jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye moja ya matrekta aliyokabidhi kama ishara kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo na mkombozi kwa wakulima katika falsafa yake ya kuzalisha kwa tija na kulisha wengine kibiashara.