Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Kilimo

CHONGOLO ATOA ONYO KALI KWA WANAONUFAIKA KINYUME CHA SHERIA NA RUZUKU YA MBOLEA

08 Nov, 2026 - 10 Nov, 2026
09:00:00 - 15:30:00
RUVUMA
ps@kilimo.go.tz

Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb), ametoa onyo kali kwa wafanyabiashara, mawakala na wote wanaojihusisha na usambazaji wa pembejeo za kilimo wanaotumia vibaya ruzuku ya mbolea inayotolewa na Serikali kwa manufaa yao binafsi.

Akizungumza tarehe 11 Novemba 2026 wakati wa kuhitimisha ziara ya kikazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, mkoani Ruvuma, Waziri Chongolo amesema kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayebainika kujinufaisha kwa njia zisizo halali kupitia ruzuku hiyo.

Amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuongeza gharama za mbolea kwa wakulima au kutumia mpango wa ruzuku kinyume na malengo yake, huku akieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea kwa bei nafuu ili kuongeza uzalishaji na tija katika Sekta ya Kilimo.

CHONGOLO ATOA ONYO KALI KWA WANAONUFAIKA KINYUME CHA SHERIA NA RUZUKU YA MBOLEA