Wakulima wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu wamebadili mtazamo wao hasi wa mbolea kuwa ni chanzo cha uharibifu wa udongo; ambapo wamepata elimu kuwa matumizi ya mbolea ni nyenzo muhimu ya kuuwezesha udongo kurudisha uhai wake na kuchochea uzalishaji wa mazao.
Hayo yamebainishwa wakati wa mafunzo waliyopatiwa na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na taasisi zake tarehe 04 Desemba 2025 mkoani humo katika kujiandaa na msimu wa kilimo wa mwaka 2025/2026.
Wakulima zaidi ya 150 katika Wilaya ya Ikungi, Mkoa wa Singida wakipatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Wizara ya Kilimo ya “Mali Shambani, Silaha Mbolea” iliyoanza mkoani humo tarehe 03 Desemba 2025.
Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Stephen Nindi ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kuhakikisha sayansi pamoja na tafiti za kilimo zinawafikia wakulima wote nchini ili kuwawezesha kuzitumia tenkolojia hizo kuzalisha kwa tija.
Dkt. Nindi amesema hayo tarehe 3 Desemba, 2025 katika ufunguzi wa Siku ya Udongo Duniani iliofanyika katika viwanja vya Nane Nane vya John Malecela vilivyopo Nzuguni jijini Dodoma, ikiwa na Kauli mbiu “Afya Bora ya Udongo kwa Miji Maridhawa".